Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
LIGI Kuu ya Azam Uganda inaendelea tena leo kwa mechi kadhaa kupigwa viwanja tofauti, macho ya wengi yakielekezwa katika mchezo kati ya mahasimu wa Jinja, Sadolin Paints na Bul FC Uwanja wa Bugembe.
Timu hizo mbili zilipokutana mara ya mwisho zilitoka sare ya 1-1, Sadolin Paints wakianza kupata bao kupitia kwa Andrew Basooma na Ivan Lubaale kuisawazishia BUL F.C.
Kwa sasa, Sadolin Paints inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi hiyo, kwa pointi zake 28 na BUL F.C ni ya tano kwa pointi zake 37.
Katika mechi nyingine, Lweza F.C iaanza kupigania kuepuka kushuka daraja watakapoifuata SC Victoria University Uwanja wa Taifa wa Nelson Mandela, Namboole.
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa Victoria University ndani ya siku mbili, baada ya Jumapili kufungwa na SC Villa 2-1 katika Robo Fainali ya Kombe la Uganda.
Timu zote mbili haziko salama katika hatari ya kushuka daraja kimahesabu. SCVU ina pointi 28 na Lweza inazo 22.
Katika Uwanja wa Jeshi wa Bombo, Simba, inayofundishwa na kocha mpya mteule Msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Moses Basena itamenyana na timu nyingine iliyo katika hatari ya kushuka daraja – Entebbe.
Wakati Simba ikiwa na pointi 25, Entebbe iko chini zaidi kwa pointi zake 14 za mechi 22. Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, Rwenshama watakuwa wenyeji wa Police F.C.
Ligi hiyo ya Azam itaendelea Ijumaa wiki hii kwa mechi kati ya Kira Young Vs Express FC Uwanja wa Namboole, Bright Stars Vs URA FC Uwanja wa Matugga, Lweza Vs Police FC Uwanja wa Wankulukuku, Soana Vs SC Villa Uwanja wa Kavumba na KCC FC Vs Vipers FC Uwanja wa Lugogo.

0 comments:
Post a Comment