NAHODHA wa Chelsea, John Terry sasa ndiye mchezaji wa nafasi za ulinzi aliyefunga mabao mengi zaidi Ligi Kuu England baada ya Jumatano kufunga katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Leicester.
Nahodha huyo wa zamani wa England alimtungua kipa Kasper Schmeichel Uwanja wa King Power jana kufunga bale la 38 tangu aanze kucheza Ligi Kuu.
Bao hilo linamfanya Terry, ambaye amefunga kila msimu katika misimu 15 iliyopita Ligi Kuu kumfikia beki wa zamani wa Everton, David Unsworth.
Kwa kuwa Terry bado yuko vizuri na anaendelea kucheza Chelsea kuna matumaini makubwa atafunga tena na kuwa beki mfungaji bora katika historia ya Ligi Kuu England.
Unsworth, ambaye aliichezea timu ya taifa ya England pia, alikuwa mkali kwa guu lake la kushoto katika kufunga.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 41 sasa, ambaye mabao yake mengi alifunga akiwa na klabu hiyo ya Merseyside, Everton, alikuwa mtaalamu wa kupiga mikwaju ya penalti na mipira ya adhabu na Terry anafuata nyayo zake vizuri.
0 comments:
Post a Comment