// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HUKUMU YA KESI YA TAMBWE NA SIMBA SC HII HAPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HUKUMU YA KESI YA TAMBWE NA SIMBA SC HII HAPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 30, 2015

    HUKUMU YA KESI YA TAMBWE NA SIMBA SC HII HAPA

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Amissi Tambwe aliwasilisha malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wake Desemba 15, 2014. Uamuzi wa kuvunja mkataba ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba ilitakiwa iwe imemlipa fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014.
    Katibu Mkuu wa Simba SC , Steven Ally alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na kuwa wameshafanya mawasiliano na wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na kupanga utaratibu wa kulipa isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya makubaliano ya malipo (Deed of Settlement).
    Amissi Tambwe amepata suluhisho la malipo ya fedha zake Simba SC
    Kamati imesikitishwa na klabu ya Simba kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa katika makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba 15, 2014.
    Klabu ya Simba inatakiwa kumlipa Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ya dola 5,000 malipo yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la dola 2,000 ili kukamilisha jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10, 2015, uamuzi ambao upande wa Simba ulikubaliana nao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUKUMU YA KESI YA TAMBWE NA SIMBA SC HII HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top