GWIJI wa Ufaransa, Thierry Henry amekandia ushangiliaji wa Javier Hernandez 'Chicharito' baada ya kufunga bao la ushindi dakika za lala salama katika Robo Fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid akisema; "Kama ameshinda Kombe la Dunia'.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid aliwanua mashabiki wa nyumbani kwa kufunga bao la ushindi baada ya kupokea pasi ya Cristiano Ronaldo zikiwa zimesalia dakika mbili baada ya kazi nzuri ya Mreno huyo.
Nyota huyo wa Mexico, Hernandez akakikimbilia kwenye kona kushangilia peke yake baada ya kufunga, lakini Henry anafikiri mshambuliaji huyo wa mkopo kutoka Manchester United, 'amepora' sifa za mchezaji mwenzake.
Javier Hernandez akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Real Madrid lililoipeleka Nusu Fainali
Henry aliiambia Sky Sports: "Ili kutenda haki kwake, hakucheza haswa. Alipewa nafasi usiku huu, lakini bado hatujui kama atacheza tena.
"Alipata nafasi kadhaa katika mchezo. Moja katika mguu wake wa kushoto na kisha nyingine katika mguu wake wa kulia. Lakini naweza kukuambia, anahitaji kumshukuru (Cristiano) Ronaldo usiku huu.
"Nafahamu alikwenda kushangilia peke yake na kila kitu, lakini anahitaji kumshukuru Ronaldo, kwa sababu kwangu alichangia pia. Ni Ronaldo ambaye alichagua kubadilisha mwelekeo wa mchezo.
Hernandez akiteleza kwenye nyasi kushangilia bao lake lililoipeleka Real Madrid Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa
"Alimuona jamaa katika nafasi nzuri, ambaye alikuwa ni Hernandez, na akampa mpira, hivyo hilo ni bao la Ronaldo. Ambacho sijapenda ni ushangiliaji wake kama ameshinda Kombe la Dunia. Alitakiwa kufunga na kugeuka kushangilia na Ronaldo.
Thierry Henry haraka alimshambulia mshambuliaji huyo wa Mexico kwa namna alivyoshangilia bao lake jana
Kwa upande wake, beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher na mchambuzi mwenzake Henry, pamoja na kusema Ronaldo ni mbinafsi, lakini akamsifu kwa alichokifanya kwani ndicho alipaswa kufanya kwa manufaa ya timu.
"Lilikuwa bao la Ronaldo kwa maana ya jitihada alizofanya kupatikana kwa bao lile, lakini Ronaldo ni wa ovyo zaidi duniani katika mambo kama yale.
0 comments:
Post a Comment