KIUNGO Jordan Henderson anataka mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki ili kusaini Mkataba mpya Liverpool.
Nahodha huyo Msaidizi wa klabu hiyo, anataka kubaki Anfield, lakini si kwa mshahara wa sasa wa Pauni 60,000 kwa wiki.
Mazungumzo juu ya mkataba mpya yanaendelea na tayari Henderson amekataa mshahara wa Pauni 80,000 kwa wiki kusaini Mkataba wa miaka mitano.
Jordan Henderson anataka Pauni 100,000 kwa wiki kusaini Mkataba mpya Liverpool
Lakini bado kuna matumaini makubwa kwa pande zote mbili kufikia mwafaka haraka iwezekanavyo na BIN ZUBEIRY inafahamu kiasi cha Pauni Milioni 5.2 kwa mwaka kitatosha kumbakiza Liverpool Henderson kwa muda mrefu.
Kiwango cha kiungo huyo kimeendelea kuimarika vizuri kuanzia Liverpool hadi timu ya taifa, England kwa misimu miwili iliyopita.
Nahodha Msaidizi wa Liverpool alifunga kwa penalti Liverpool ikilala 4-1 mbele ya Arsenal Jumamosi
Henderson, anafanya suala la Mkataba wake liwe kutatuliwa kwa sababu anatarajiwa kuteuliwa Nahodha Mkuu Anfield, mara Steven Gerrard atakapoondoka kwenda LA Galaxy mwishoni mwa msimu.
Akizungumza mwezi uliopita, Henderson alisema: "Napenda kucheza soka Liverpool na ninataka kubaki huko kwa miaka mingi,".
"Kuhusu Mkataba wangu, nafikiri kila mmoja pia atafanya jambo la maana, lakini kwangu, ninaamuachia wakala wangu amalizane na klabu,"alisema.
0 comments:
Post a Comment