KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard ameendelea kung'ara katika soka ya Uingereza baada ya kuteuliwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA).
Mchezaji huyo nyota wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24, ameifungia Chelsea mabao 18 katika mashindano yote msimu huu, akiiwezesha kutwaa taji la Kombe la Ligi maarufu kama Capital One na kuwasogeza karibu kabisa na ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.
Alipewa tuzo hizo kutokana na soka yake 'babu kubwa' katika ukumbi wa hoteli ya Grosvenor mjini London usiku wa kuamkia leo.
Ushindi katika mechi mbili zjijazo za Chelsea dhidi ya Leicester na Crystal Palace nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge utaifanya Chelsea ijihakikishie ubingwa ligi ikiwa inaendelea.
Eden Hazard akiwa na tuzo yake ya PFA usiku wa kuamkia leo London
http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3056557/Eden-Hazard-wins-PFA-Player-Year-award-following-stellar-season-champions-elect-Chelsea.html#ixzz3YTkHuPJ2
0 comments:
Post a Comment