// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HANS POPPE: HATUWAZUII WACHEZAJI KULA RAHA NA MADEMU, TUNATAKA WAFUATE NYAYO ZA SAMATTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HANS POPPE: HATUWAZUII WACHEZAJI KULA RAHA NA MADEMU, TUNATAKA WAFUATE NYAYO ZA SAMATTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    HANS POPPE: HATUWAZUII WACHEZAJI KULA RAHA NA MADEMU, TUNATAKA WAFUATE NYAYO ZA SAMATTA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hawaingilii maisha binafsi ya wachezaji wao, lakini wanaweza kuwashauri kwa faida ya maisha yao wenyewe.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, Hans Poppe amesema kwamba wachezaji wote wa SImba SC ni wakubwa kisheria kwa sababu wamefikisha miaka 18 au zaidi, hivyo hao ni watu wazima.
    “Umri wa miaka 18 mtu anapiga kura. Ni mtu  mzima huyo, si mtoto. Lakini kwa kuwa sisi tuna watoto tena wakubwa zaidi yao, ni wajibu wetu kuwashauri tunapoona wanakosea, au wanataka kupotea,”.
    Hans Poppe (kushoto) amesema Simba SC hawaingilii maisha binafsi ya wachezaji wao

    “Hatuingilii maisha binafsi ya mchezaji. Naomba hiyo ieleweke. Mchezo wa mpira unahitaji utimamu wa mwili. Sasa unapoona mchezaji anataka kuharibu utimamu wake wa mwili, si vibaya ukamshauri,” amesema.
    Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema hakatazwi mchezaji wa Simba SC kuwa na mpenzi, lakini anapaswa kuzingatia kwamba mwanamke havurugi ratiba zake za mazoezi na kazi kwa ujumla.
    “Inapotokea mwanamke akakuteka akili hadi ukawa unashindwa kuzingatia programu za mazoezi hiyo ni mbaya. Lakini kama unakuwa na mwanamke wako, unajitunza, unajibidiisha kukuza kiwango chako, sisi hatuwezi kuwa maneno na wewe,”ameongeza.    
    Poppe amewaasa wachezaji wa Simba SC kujitambua na kuwa na kiu na malengo ya kufika mbali kisoka.
    Poppe amemtolea mfano mshambuliaji Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anachezea TP Mazembe ya DRC, kwamba kama angejiruhusu kutekwa akili na mwanamke alipokuwa Simba SC, asingefikia mafanikio aliyonayo sasa.
    “Sasa Samatta anazungumzia kwenda Ulaya, lakini ni juzi tu hapa alikuwa Simba SC tena kijana mdogo na mchezaji wa timu za vijana kama hawa tulionao sasa. Dhahiri huyu alikuwa ana malengo na akazingatia miiko na maadili ya soka ndiyo maana anafanikiwa,”.
    “Sasa hii inawezekana hata kwa wachezaji wengine chipukizi tulionao sasa, kama watajiwekea malengo na kuzingatia miiko na maadili ya soka,”amesema Poppe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPPE: HATUWAZUII WACHEZAJI KULA RAHA NA MADEMU, TUNATAKA WAFUATE NYAYO ZA SAMATTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top