MSHAMBULIAJI Radamel Falcao anaweza kusaini Mkataba wa moja kwa moja kuendelea kuichezea Manchester United, baada ya kugundulika kwamba Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ed Woodward alifanya mazungumzo na Monaco Jumapili juu ya mustakabali wa nyota huyo.
Falcao, ambaye amefunga mabao manne United tangu atue kwa mkopo wa muea mrefu wa msimu kutioka Monaco, alishindwa kufurukuta Uwanja wa Stamford Bridge dhidi ya Chelsea Jumamosi.
Lakini Woodward amemuambia Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim Vasilyev Jumapili iliyopita kwamba 2atafanya uamuzi wa kumchukua moja kwa moja au kuachana naye mwishoni mwa msimu.
Radamel falcao ameshindwa kung'ara Man United
0 comments:
Post a Comment