// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ETOILE WATAMKUTA COUTINHO YUKO ‘MOTO BATI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ETOILE WATAMKUTA COUTINHO YUKO ‘MOTO BATI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Tuesday, April 07, 2015

    ETOILE WATAMKUTA COUTINHO YUKO ‘MOTO BATI’

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    HALI ya kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mbrazil Andrey Coutinho inazidi kuimarika taratibu na bila shaka hadi mchezo dhidi ya Etoile du Sahel, atakuwa fiti kwa asilimia 100.
    Yanga SC itakutana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika katikati ya mwezi huu mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye Tunis.
    Na Coutinho ambaye hajacheza mpira mwezi wote uliopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti baada ya kuumia akiichezea timu hiyo mjini Mbeya, anatarajiwa kuwa fiti kabisa.
    Andrey Coutinho kushoto sasa anafanya mazoezi kikamilifu Yanga SC

    Coutinho ameanza programu kamili ya mazoezi Yanga SC na yeye mwenyewe amesema anafurahishwa na jinsi hali yake inavyoendelea.
    “Ninaendelea vizuri, natumaini baada ya mechi mbili nitakuwa katika ubora wangu kabisa. Hata sasa najisikia vizuri kabisa na nina hamu ya kucheza tena,”amesema.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ETOILE WATAMKUTA COUTINHO YUKO ‘MOTO BATI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry