Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
ETOILE du Sahel watahitaji kuwaona tena beki Mbuyu Twite na kiungo mshmbuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa kabla hawajaamua cha kufanya.
Etoile wameonekana kuvutiwa na wachezaji hao wawili wa Yanga SC baada ya mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baina ya timu hizo Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Vionogzi wa Etoile walimuuliza mwandishi wa habari hizi kuhusu wachezaji hao wawili juu ya umri wao na kama wanacheza timu za taifa. Na wakafurahi zaidi walipoambiwa Mrisho Ngassa atakuwa mchezaji huru mwezi ujao.
Hata hivyo, Rais wa Etoile, Ridha Charfeddine; “Tunahitaji kuwaona tena Tunisia,”.
Lakini kiungo Mcameroon wa Etoile, Frank Kom alimfuata Twite baada ya mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na kuzungumza naye zaidi ya dakika tano.
“Nimevutiwa na huyu ni mchezaji mzuri sana, nimekuja kusalimiana naye ili kujuana, mchezaji mzuri sana,”alisema Kom alipoulizwa na BIN ZUBERIY juu ya mazungumzo yake na Twite.
Yanga na Etoile zitarudiana mwishoni mwa wiki ijayoround Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia, baada ya sare ya juzi na mshindi wa jumla ataingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho akicheza na moja ya timu zitakazotolewa katika Ligi ya Mabingwa.
Etoile sasa ndiyo wana nafasi kubwa ya kusonga mbele baada ya sare ya mabao ugenini, kwani Yanga SC watalazimika kushinda mjini Sousse, au sare ya zaidi ya bao 1-1 ili wawatoe Waarabu hao.

Mbuyu Twite (kushoto) na Frank Kom walizungumza kwa dakika kadhaa juzi |
Mrisho Ngassa kulia akiwania mpira dhidi ya beki wa Etoile du Sahel |
Lakini kiungo Mcameroon wa Etoile, Frank Kom alimfuata Twite baada ya mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na kuzungumza naye zaidi ya dakika tano.
“Nimevutiwa na huyu ni mchezaji mzuri sana, nimekuja kusalimiana naye ili kujuana, mchezaji mzuri sana,”alisema Kom alipoulizwa na BIN ZUBERIY juu ya mazungumzo yake na Twite.
Yanga na Etoile zitarudiana mwishoni mwa wiki ijayoround Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia, baada ya sare ya juzi na mshindi wa jumla ataingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho akicheza na moja ya timu zitakazotolewa katika Ligi ya Mabingwa.
Etoile sasa ndiyo wana nafasi kubwa ya kusonga mbele baada ya sare ya mabao ugenini, kwani Yanga SC watalazimika kushinda mjini Sousse, au sare ya zaidi ya bao 1-1 ili wawatoe Waarabu hao.
0 comments:
Post a Comment