WAPINZANI wa Yanga SC katika Kombe la Shirikisho la Afrika, Etoile du Sahel (pichani juu) wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Esperance katika Ligi Kuu ya Tunisia jioni ya leo.
Katika mchezo huo wa Ligue 1 uliofanyika Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Etoile bao moja lilipatikana kila kipindi.
Wenyeji, Etoile walitangulia kupata bao kupitia kwa Youssef Mouihbi dakika ya 27, kabla ya Haythem Jouini kuwasawazishia Esperance dakika ya 48.
Matokeo hayo yanaifanya Etoile iendelee kukamata nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 51, nyuma ya Club Africain yenye pointi 52, ingawa timu zote zimecheza mechi 25.
Esperance inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake 50 baada ya kucheza mechi 25 pia, wakati CS Sfaxien ni ya nne kwa pointi zake 41 za mechi 24.
Esperance inashiriki Ligi ya Mabingwa na wiki ijayo itarudiana na El Merreikh baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza Sudan. Etoile ilianza kwa sare ya 1-1 ugenini na Yanga.

0 comments:
Post a Comment