NEMBO ya Shirika la ndege la Emirates itakuwa maarufu zaidi katika anga ya michezo duniani.
Jumanne, BIN ZUBEIRY iliandika kwamba kampuni hiyo ya Dubai inatarajiwa kuingia Mkataba wa kihistoria na Kombe la FA, ambao utaifanya michuano hiyo mikongwe ya mtoano duniani ibadilishwe jina na kuwa Kombe la Emirates la FA.
Mkataba huo wa Pauni Milioni 30 utaongeza hadhi na thamani ya michuano hiyo ya England. BIN ZUBEIRY inakuletea mikataba mingine ambayo shirika hilo limeingia katika sekta ya michezo.
Arsenal walishinda Kombe la FA mwaka jana, sasa michuano hiyo itaitwa Emirates FA Cup
EMIRATES WALIVYOJIKITA KWENYE MICHEZO'
SOKA;
Arsenal na Uwanja wa Emirates
Thamani ya Mkataba: Pauni Milioni 150
Arsenal ilipata Mkataba mnono wa udhamini katika historia ya soka ya Uingereza mwaka 2004 kufuatia kusaini Mkataba wa miaka 15 wenye thamani ya Pauni Milioni 100 na shirika hilo la kimataifa la ndege la nchini Dubai.
Mkataba huo ulihusu haki za kuupa jina la Emirates Uwanja wa Arsenal wenye kuchukua watu 60,000 na kuweka pia kwenye jezi ya klabu hiyo neno 'Fly Emirates' wakiwapiku O2 waliokuwa wadhamini wa klabu kuanzia msimu wa 2006-07 katika Ligi Kuu.
Desemba 2012, Mkataba mpya wa Pauni Milioni 150 ulikubaliwa kuendeleza uhusiano wa pande hizo mbili hadi mwishoni mwa msimu wa 2018-2019.
Uwanja wa Arsenal umepewa jina Emirates baada ya Mkataba wa fedha nyingi mwaka 2004
Kombe la Emirates
Kombe la Emirates
Michuano ya kujiandaa na msimu mpya inaitwa ilianza mwaka 2007 na hufanyika katika Uwanja wa Arsenal, Emirates. Katika kipindi hicho timu kama Real Madrid, Inter Milan na Juventus zimeingia kwenye mashindano hayo kucheza mechi mbili kila timu kuwania Kombe hilo.
Kombe la Emirates limekuwa likirushwa la BT Sport kwa Uingereza na nchi nyingine duniani, hivyo kukuza umaarufu wa shirika hilo la ndege.
Shule za soka za Arsenal, Dubai
Kwa ushirikiano Emirates na Arsenal walianzisha shule za soka mwaka 2009 na zinadhaminiwa na shirika hilo la ndege. Shule hizo ni kwa ajili ya watoto wa kike na wa kiume wa umri wote.
Alexis Sanchez (kushoto) akicheza Kombe la Emirateskati ya Arsenal na Monaco mwezi Agosti
AC Milan
AC Milan
Thamani ya Mkataba: Pauni Milioni 80
Emirates ilivamia katika soka ya Italia mwaka 2010 baada ya kuingia Mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Pauni Milioni 52 na AC Milan. Mwaka 2014, klabu hiyo ya Serie A ilisaini Mkataba mpya mnono na shirika hilo maarufu la ndege, ambao utafikia tamati msimu wa 2019-2020.
Mkataba huo mpya wa miaka mitano, uliripotiwa kuwa na thamani ya pauni Milioni 80, wakati Mkataba huo mpya pia unahusu kuupa jina Uwanja wa Milan, San Siro, kudhamini timu ya vijana ya klabu na haki za masoko.
Emirates wameweka fedha zao katika ya Italia kuanzia mwaka 2010 walipoanza kuidhamini AC Milan
Hamburg
Hamburg
Thamani ya Mkataba: Pauni Milioni 17
Uhusiano wa Hamburg na Emirates ulianza mwaka 2006 baada ya timu hiyo ya Bundesliga kukubali Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 11. Mwezi Februari mwaka 2012, Mkataba huo ulisainiwa upya kwa miaka mitatu zaidi huku ukiwa kipengele cha kuurefusha hadi mwaka 2016.
Mkataba wa Pauni Milioni 5 kwa mwaka umeshuhudia nembo ya Emirates ikizipamba jezi za klabu hiyo na Uwanja wa Hamburg, Imtech Arena.
Vigogo wa Bundesliga, Hamburg wamekuwa na uhusiano na Emirates tangu mwaka 2006
New York Cosmos
New York Cosmos
Thamani ya Mkataba: Pauni Milioni 5
The New York Cosmos iliungana na Arsenal na Real Madrid kwa kusaini Mkataba na shirika hilo la ndege mwaka 2013.
Nembo ya Emirates inapamba jezi za timu hiyo ambayo Pele amewahi kuichezea hadi mwaka 2018 baada ya kuongezwa miaka miwili mwaka jana. Cosmos imeripotiwa kuingiza wastani wa Pauni Milioni 1 kwa mwaka.
Paris Saint-Germain
Thamani ya Mkataba: Pauni Milioni 90
Wachezaji wa PSG walianza kuvaa nembo ya Emirates mwaka 2006 wakati Mkataba wa Pauni Milioni 3.5 kwa mwaka ulipoanza.
Kufuatia mafanikio ya karibuni ya klabu hiyo, Mkataba mpya unatarajiwa kuwa na thamani ya Pauni Milioni 18 kwa msimu ambao utawafanya wadumu na Emirates mwaka 2018.
Kufuatia mafanikio ya karibuni ya klabu hiyo, Mkataba mpya unatarajiwa kuwa na thamani ya Pauni Milioni 18 kwa msimu ambao utawafanya wadumu na Emirates mwaka 2018.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya Habari, makubaliano ya Pauni Milioni 90 ya Mkataba wa PSG, yanamaanisha hicho ni kiwango cha chini kulinganisha na klabu za Ligi Kuu England.
Edinson Cavani akishangilia na jezi ya PSG yenye nembo ya 'Fly Emirates' ambao wamekuwa wakiidhamini timu hiyo mwaka 2006
Real Madrid
Real Madrid
Thamani ya Mkataba: Pauni Milioni 105
Mwaka 2013, Emirates ilifanikiwa kuingia Mkataba wa udhamini na klabu kubwa duniani, Real Madrid.
Hakuna taarifa rasmi za dau la Mkataba zilizowahi kutolewa, lakini inaelezwa thamani yake ni Pauni Milioni 21 kwa mwaka.
Mkataba wa shirika hilo la ndege unaifanya Madrid iwapiku wapinzani wao, Barcelona ambao wanadhaminiwa na Qatar Foundation kwa dau la Pauni Milioni 20 kwa msimu tangu mwaka 2016.
Mkataba wa shirika hilo la ndege unaifanya Madrid iwapiku wapinzani wao, Barcelona ambao wanadhaminiwa na Qatar Foundation kwa dau la Pauni Milioni 20 kwa msimu tangu mwaka 2016.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid alisajiliwa kutokana na fedha za Mkataba mnono wa Emirates mwaka 2013
Shirikisho la Soka Asia
Shirikisho la Soka Asia
Emirates ilikuwa mdhamini wa kwanza rasmi wa Shirikisho la Soka barani Asia mwaka 2002.
Ligi ya kulipwa ya Zain Saudi (Saudi Arabia)
Mwaka 2011, Emirates ilisaini Mkataba wa miaka mitatu na nusu kudhamini Ligi Kuu ya Saudi Arabia ijulikanayo kama Zain Saudi League.
0 comments:
Post a Comment