// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BINGWA LIGI YA WANAWAKE SOKA DAR ZAWADI KIBAO NA 'MPUNGA MNENE' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BINGWA LIGI YA WANAWAKE SOKA DAR ZAWADI KIBAO NA 'MPUNGA MNENE' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    BINGWA LIGI YA WANAWAKE SOKA DAR ZAWADI KIBAO NA 'MPUNGA MNENE'

    Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
    CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA), kimetja zawadi kwa washindi wa michuano ya ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam inayoendelea katika viwanja mbalimbali Jijini.
    Mwenyekiti wa chama hicho Almas Kasongo,amesema zawadi hizo zitatolewa kwa mshindi wa kwanza na wapili,mchezaji bora wa mashindano,mfungaji bora,kipa bora,timu yenye nidhamu na mwamuzi bora.
    Bingwa atazawadiwa Kombe, jezi seti moja na  Sh. 1, 500,000, wakati mshindi wa pili atapata jezi seti moja na kiasi cha Sh 700, 000.

    Mchezaji bora wa mashindano atazawadiwa kiasi cha Sh 200, 000, Mfungaji bora Sh. 150, 000 sawa na Kipa bora, wakati timu yenye nidhamu bora itazawadiwa Sh 400, 000 , huku mwamuzi bora akiondoka na Sh. 200,000.
    Ligi hiyo yenye jumla ya timu 8 imeanza kutimua vumbi Jumapili ya Aprili 19, 2015, kwa mchezo wa ufunguzi uliozikuwanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens,na kushuhudiwa Ever-Green ikichomoza na ushindi wa kishindo wa mabao 5-1, yaliyofungwa na Sherida Boniface dakika ya 7,19na 39,na mengine yakifungwa na Donicia Daniel katika dakika ya 60 na 65,na lile la kufutia machozi kwa Temeke Squad likifungwa na Aisha Juma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BINGWA LIGI YA WANAWAKE SOKA DAR ZAWADI KIBAO NA 'MPUNGA MNENE' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top