// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BANDARI WAFUMULIWA PASAKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BANDARI WAFUMULIWA PASAKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Monday, April 06, 2015

    BANDARI WAFUMULIWA PASAKA

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    BANDARI FC wamemaliza pasaka yao na kichapo cha magoli 2-0 na Ulinzi Stars kwenye mechi ya ligi kuu Kenya, KPL, iliyogaragazwa ugani Mbaraki alasiri ya leo.
    John Makwata aliipa Ulinzi bao la kwanza dakika ya 53 akimalizia krosi murwa yake Oliver Ruto aliyetokezea pembeni kisha Oscar Wamalwa akapigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Bandari dakika ya 60. Chipukizi huyo alitumia uzembe wa mabeki Shariff Mohammed na Humphrey Okot wa kutoondoa uchafu langoni kwa kuwachilia pande la shuti hadi nyavuni kipa Wilson Obungu akibakia kuhesabu ndege baharini.

    Mbinu za vijana wa Twahir Muhiddin kuhifadhi rekodi yao ya kutopoteza ngarambe yoyote nyumbani hazikufua dafu David King'atua, Mganda George Abege na Victor Ndinya wakipoteza nafasi za kuhesabu.
    Katika matokeo ya wikiendi, Jesse Were alicheka na nyavu mara mbili na kuinusuru Tusker FC kutoka kwa mtego wa Chemelil Sugar Jumamosi ugani Chemelil Sports Complex. Hamisi Mwinyi  na Daniel Mutahi walikuwa wameiweka Chemelil kifua mbele.
    Kwingineko siku ya jumapili, Western Stima waliibuka washindi dhidi ya Sofapaka kwao Kisumu kwa magoli 3-2, Mathare United 2-0 City Stars, Muhoroni Youth 1-1 Ushuru FC, Nakuru AllStars 1-0 SoNy Sugar huku Thika United ikivuna pointi moja dhidi ya mabingwa mara 12 AFC Leopards katika uchanjaa wa Mumias.
    Ni Jumapili iyo iyo mabingwa watetezi Gor Mahia waliondolewa katika mechi za mabingwa barani Afrika na AC Leopard ya Congo magoli 2-0 kwa jumla baada ya 1-0 mjini Dolisie.
    Mechi za ligi kuu ya Shirikisho la Soka Kenya, FKF PL, vile vile zilisakatwa wikiendi iliyopita na haya ndio matokeo yake.
    Jumamosi
    Kakamega Homeboyz 0-0 Kariobangi Sharks
    FC Talanta 1-2 Zoo Kericho
    Oserian 2-0 St. Joseph
    Moyas 0-2 Ligi Ndogo
    Nzoia United 1-1 Shabana FC
    Jumapili
    Nairobi Stima 0-3 Bidco United
    Posta Rangers 2-0 Agrochemicals
    West Kenya 2-1 Finlays Horticulture
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BANDARI WAFUMULIWA PASAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry