PAMOJA na kwamba bondia Floyd Mayweather ataongeza dola za Kimarekani Milioni 180 katika akaunti yake ya benki Jumamosi usiku, kuna wasiwasi kwamba mwanamichezo huyo tajiri duniani atabaki mtupu hana senti hata moja siku moja.
Baba wa Mayweather - Floyd Snr, ambaye pia ni kocha mwanawe huyo - ni miongoni mwa wenye hofu hiyo kwamba jamaa huyo ambaye anajiita Money, yaani anaweza kugeuka 'fukara' atakapoacha kupanda ulingoni.
Wasiwasi huo unaletwa na mfumo wa maisha ya matanuzi na kutumia sana fedha wa Mayweather ambaye keshokutwa anapigana na Manny Pacquiao katika 'Pambano la Karne'.
Floyd Mayweather Snr (kushoto) anahofia mwanawe atafilisika akiendekeza matanuzi
Utajiri wake unatarajiwa kufika dola Milioni 600 kutoka dola Milioni 420 za sasa anazokadiriwa kuwa nazo kutokana na namna anavyoingiza fedha.
Vipi mtu anaweza kufilisika akiwa na kiasi hicho cha fedha?
Mayweather Snr anafafanua; "Waangalie mamilionea ambao wanafilisika. Unapokuwa na fedha nyingi kiasi hiki, huwezi kuzimudu.
"Milioni mia moja nyingine (dola), milioni mia mbili zinaongezeka juu ya zile ulizonazo, inaonekana kama kitu kirefu. Lakini unaweza kufanyia kitu chochote hizo fedha.
"Kama Floyd anazifanyia mambo sahihi, anatakuwa njema maisha yake yote ya baadaye. Lakini huwezi kutarajia kuwa na fedha yoyote ndani ya miaka miwili ikiwa unafanya matanuzi, unakula raha, safari, magari na wanawake. Wapiganaji wengi wamefilisika kwa namna hiyo,".
Mfumo wa maisha wa Mayweather Jnr ni matanuzi kwa kwenda mbele bila kujiuliza wala kuhofia.
Magari mia moja la muuza magari wa Las Vegas miaka 18, likiwemo na 16 Rolls Royces sambamba na Bugattis vyote vinagharimu dola Milioni 1-3.
Saa ya kifahari inayosemekana kuwa na thamani ya nusu milioni. Kwenda kununua vito vya thamani, viliripotwa kumgharimu zaidi ya dola Milioni 6 kwa siku moja mjini New York.
Wabunifu wengi wa viatu vya kimichezo anavyovyaa kila pea, huwachukulia chumba cha suti katika hoteli za kifahari walale kama zawadi kwa kazi yao.
Kutoka kushoto: Ferrari 599 GTB Fiorano, Porsche 911 Turbo S, Lamborghini Aventador, Ferrari 458 Spider, Ferrari 458 Spider. Bugatti Grand Sport, Bugatti Veyron, Bugatti Veyron na ndege binafasi yenye thamani ya dola Milioni 30
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 baada ya pambano la Jumamosi atabaki na pambano moja tu kumaliza Mkataba wake wa mapambano sita na na Showtime, ambalo amepanga kupigana Septemba. Litakuwa pambano lake la mwisho.
PICHA ZAIDI NENDA:
0 comments:
Post a Comment