Na Philipo Chimi, SHINYANGA
BAADA ya Mwadui FC kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao, Wilaya ya Kishapu imepania kupeleka timu zadi juu na sasa mkakati uliopo ni wa kuiinua Watumishi FC.
Chama cha Soka Kishapu (KDFA) kimeahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Watumishi FC baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa wa Shinyanga msimu huu wa 2015, ili ipande zaidi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY juzi mjini hapa, Katibu Mkuu wa KDFA, Mussa Salum amesema kwamba licha ya timu hiyo kuwa chini ya usimamizi mzuri wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, chama pia kitatoa ushirikiano wa kila namna katika timu hiyo, ili kuhakikisha inafanya vizuri katika Ligi Daraja la pili Tanzania Bara msimu ujao.
Mussa ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau na wapenzi wa soka wilayani humo na mkoa wote wa Shinyanga kuendelea kuisapoti timu hiyo katika maadalizi ya michuano mingine inayofuata.
Timu nyingine ya Kishapu, Mwadui FC imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
Watumishi FC imeungana na Bulyankulu FC ya Kahama, ambayo imeshindwa kupanda kwenda Daraja la Kwanza msimu huu. Watumishi FC ilichukua ubingwa wa Mkoa wa Shinyanga baada ya kuichapa Ambassador FC ya Kahama mabao 5-4 katika fainali ya kuwania ubingwa wa mkoa huo iliyopigwa jumapili Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Mwadui FC itacheza Ligi Kuu msimu ujao |

0 comments:
Post a Comment