KLABU ya Arsenal inasikilizia msimamo wa mwisho wa Petr Cech juu ya mustakabali wake kabla ya haijamtokea kipa huyo huyo wa Chelsea.
Kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech anajipanga kuondoka Stamford Bridge mwishoni mwa msimu, na klabu hiyo inajiandaa kuachana na kipa huyo lakini kwa dau la Pauni Milioni 10 au zaidi.
Lakini kwa Cech kuhamia Arsenal, wapinzani wa Chelsea linaweza kuwa jambo gumu.
Cech, aliyejiunga na Chelsea mwaka 2004, amecheza mechi nne tu za Ligi Kuu England msimu huu
Na Gunners wanataka kujiridhisha wana nafasi nzuri ya kumsajili kipa huyo, kabla ya kumtokea, huku Chelsea ikitarajiwa kutokuwa tayari kuwauzia silaha wapinzani.
Cech alisema wiki iliyopita kwamba hataki kuona msimu ujao anaendelea kuwa kipa wa pili nyuma ya Thiabut Courtois Uwanja wa Stamford Bridge.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 amepoteza nafasi kikosi cha kwanza The Blues tangu kurejeshwa kwa Mbelgiji huyo msimu huu, akiwa amedaka mechi nne tu za Ligi Kuu ya England, huku zaidi akichezeshwa kwenye mechi za vikombe.
0 comments:
Post a Comment