Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC kilitua usiku wa jana Dar es Salaam na moja kwa moja kuunganisha Bagamoyo, Pwani kwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya mahasimu, Simba SC Jumapili wiki hii.
Yanga SC iliwasili ikitokea Botswana ambako ilikwenda kucheza mechi ya marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji BDF XI.
Katika mchezo huo uliofanyika Ijumaa usiku, Yanga SC ilifungwa mabao 2-1, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani Dar es Salaam.
Na baada ya kutua tu, kikosi kizima, kasoro mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kilielelekea Bagamoyo kwa kambi ya maandalizi ya pambano la watani.
Ngassa anatarajiwa kuungana na wenzake leo, baada ya kuomba udhuru wa kushughulikia masuala yake binafasi mapema leo.

Mrisho Ngassa kulia akizungumza na kocha Charles Boniface Mkwasa. Mchezaji huyo ataungana na wenzake kambini Bagamoyo leo baada ya kutatua masuala yake binafsi mapema |
Na baada ya kutua tu, kikosi kizima, kasoro mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kilielelekea Bagamoyo kwa kambi ya maandalizi ya pambano la watani.
Ngassa anatarajiwa kuungana na wenzake leo, baada ya kuomba udhuru wa kushughulikia masuala yake binafasi mapema leo.
0 comments:
Post a Comment