MKONGWE Xavi ameamua kwenda kumalizia soka yake katika klabu ya Al Sadd ya Qatar ambako Mtanzania, Mwinyi Kazimoto (pichani kushoto) anacheza, na anatarahjiwa kusaini Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 22 mjini Doha wiki hii.
Nahodha huyo wa Barcelona pia ataanza kukochi kizazi cha wachezaji watakaoichezea Qatar mwaka 2022 wakati wa Kombe la Dunia katika akademi ya Aspire.
Mchezaji huyo menye umri wa miaka 35 ameichagua kwenda Qatar badala ya ofa za klabu dada ya Manchester City, New York City ya Marekani.
Malipo ya Pauni Milioni 7.5 kwa mwaka yanadhaniwa kumshawishi mchezaji huyo- lakini pia na ushauri wa gwiji wa zamani wa Hispania, Raul ambaye alichezea Al Sadd kuanzia mwaka 2012 hadi 2014 alipohamia New York Cosmos. Kiungo, Kazimoto anachezea Al Markhiya ya Daraja la Pili Qatar.
Xavi anatarajiwa kuwsaini Mkataba wa miaka mitatu Al Sadd kwa Pauni Milioni 22 mjini Doha wiki hii
0 comments:
Post a Comment