// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WANASOKA WA ZAMANI TANGA WAMSHAWISHI PROFESA MUHONGO AGOMBEE URAIS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WANASOKA WA ZAMANI TANGA WAMSHAWISHI PROFESA MUHONGO AGOMBEE URAIS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 21, 2015

    WANASOKA WA ZAMANI TANGA WAMSHAWISHI PROFESA MUHONGO AGOMBEE URAIS

    Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
    UMOJA wa wachezaji wa zamani wa Tanga na baadhi wa Dar es Salaam wameungana kuanzisha kampeni ya kumshawishi aliyekuwa Waziri wa Nishati Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    Wakizungumza na BIN ZUBEIRY leo mjini Tanga, wachezaji hao walioongozwa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Omar Zimbwe wamesema Profesa Muhongo ni mwanamichezo mwenzao wa zamani na mtu mwenye elimu na uwezo mkubwa.



    Kutoka kushoto waliosimama, Mohamed Kampira, Joshua Mwalusamba, Salim Bawaziri, Said Korongo, Abdi Banda, Lawrence Mwalusako, Omar Karupa, Razack Yussuf na Douglas Muhani. Kutoka kushoto walioketi; John Lyimo, Shaaban Katwila, Omar Zimbwe, Mbwana Abushiri, Mweri Simba na Hemed Mussa wakiwa Nyinda Executive jana baada ya Mkutano wao.

    Zimbwe amesema kwamba Muhongo ni mwanasoka mwenzao wa zamani mwenye elimu ya kiwango cha juu na uwezo mkubwa wa kuongoza nchi.
    “Sisi wanamichezo tunaungana kumshawishi mwanamichezo mwenzetu huyu agombee Urais wa Tanzania. Tunamuomba ajitokeza kuomba ridhaa ya CCM kwanza,”amesema Zimbwe.
    Wachezaji wengine wa zamani wa Tanzania waliowika klabu za Dar es Salaam kama Lawrence Mwalusako na Shaaban Katwila nao walikuwepo katika Mkutano uliofanyika hoteli ya Nyinda Executive, Tanga leo.
    Mwalusako ambaye kama Katwila waliwika Yanga SC, amesema anawaunga mkono wachezaji wa Tanga kwa sababu Profesa Muhongo ni mtu safi.
    “Mimi ni mchezaji msomi na mbali na kucheza kwa kiwango cha juu hadi timu ya taifa, nimekuwa kocha na kiongozi wa klabu kubwa na TFF,”. “Nasema namjua Profesa Muhongo ni mtu safi, nami naungana na wenzangu wa Tanga kumshawishi aombe ridhaa ya CCM kugombea Urais,”amesema Mwalusako.
    Katwila pia amesema kwamba anamfahamu Profesa Muhongo ni mtu safi, msomi na mchapakazi ambaye anaweza kuivusha Tanzania katika mafanikio.
    Wachezaji wengine waliokuwepo kwenye mkutano huo ni Mohamed Kampira, Joshua Mwalusamba, Salim Bawaziri, Said Korongo, Abdi Banda, Omar Othman Karupa, Razack Yussuf na Douglas Muhani, John Lyimo, Shaaban Katwila, Mbwana Abushiri, Mweri Simba, Juma Mgunda na Hemed Mussa.
    Januari mwaka huu, Profesa Muhongo alijiuzulu wadhifa wake Wizara ya Nishati na Madini aliotumikia tangu mwaka 2012 kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegera Escrow. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WANASOKA WA ZAMANI TANGA WAMSHAWISHI PROFESA MUHONGO AGOMBEE URAIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top