KLABU za Ligi Kuu ya England zitachangia Pauni Bilioni 1 kwa zaidi ya miaka mitatu kwa klabu nyingine za madaraja ya chini nchini humo.
Katika fedha hizo kila klabu itanufaika kwa Pauni Milioni 50, ambazo zitakwenda kwenye maeneo matano ya mchezo huo.
Kiwango hicho kimekubaliwa jana Alhamisi katika kongamano la klabu za Ligi Kuu— ukiwa mkutano wa kwanza tangu wavune dili la Pauni Bilioni 5 la haki za Televisheni.
Mtendaji Mkuu wa Ligui Kuu England, Richard Scudamore amesema klabu za ligi hiyo zitachangia maendeleo ya soka nchini humo
Klabu za Ligi Kuu England zimekubaliana jana kuchangia Pauni Bilioni 1 kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini humo
Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu, Richard Scudamore amesema: "Huwezi kunipatia mimi mchezo mwingine ambao unajifunga kutoa mchango mkubwa namna hii,".
Miradi iliyolengwa katika fedha hizo ni uwekezaji katika soka ya vijana, vifaa na kusaidia moja kwa moja ligi za chini.
0 comments:
Post a Comment