URENO imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Serbia katika mchezo wa Kundi I kufuzu Fainali za Ulaya, Euro 2016 usiku huu.
Ricardo Carvalho aliifungia Ureno bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 10, kabla ya Nemanja Matic kuisawazishia Serbia dakika ya 61.
Bao la ushindi la Ureno iliyoongozwa na Nahodha wake na Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo lilifungwa na Fabio Coentrao dakika ya 63.
Kikosi cha Ureno kilikuwa; Rui Patricio, Bosingwa, R Carvalho/Fonte dk17, Alves, Eliseu, Moutinho, Tiago Mendes, Coentrao/Quaresma dk78, Nani, Danny/W Carvalho dk86 na Ronaldo.
Serbia: Stojkovic, Basta, Ivanovic, Nastasic, Kolarov, Petrovic, Matic, Markovic/Djuricic dk65, Ljajic, Tadic na Mitrovic.
Cristiano Ronaldo akimhadaa beki wa Chelsea na Serbia,Branislav Ivanovic katika mchezo wa leo mjini Lisbon
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3017133/Portugal-2-1-Serbia-Cristiano-Ronaldo-Group-I.html#ixzz3VoM7eRtb
0 comments:
Post a Comment