Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya soka ya ufukweni ya Tanzania, imeanza vibaya Raundi ya Pili ya michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, baada ya kufungwa mabao 6-2 na Misri katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni, Dar es Salaam jioni ya leo.
Matokeo hayo yanamaanisha, Tanzania ina mzigo wa kupanda mlima, kwenda kushinda kwa wastani wa mabao matano zaidi ugenini katika mchezo wa marudiano wiki ijayo.
Katika mchezo wa leo, Tanzania ilianza vizuri na kuongoza robo ya kwanza kwa mabao 2-1, kabla ya kibao kuwageukia robo ya pili na kutoka wakiwa nyuma kwa mabao 3-2.
Robo ya tatu jahazi la Tanzania inayofundishwa na beki wa zamani wa kimataifa nchini, John Jacob Mwansasu aliyewika Yanga SC, lilizidi kuzama baada ya kumaliza ikiwa nyuma kwa mabao 4-2.
Katika Robo ya mwisho ndipo Tanzania ilitota kabisa na kuongezwa mabao mengine mawili, hivyo kulala 6-2.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi na Mwalimu Akida, wakati mabao ya Misri yalifungwa na Islam Ahmed, Yahia Ally manne na Mohammed Faway.
Kwa ujumla, Tanzania ilizidiwa na Misri na ilionekana dhahiri zimekutana timu mbili za viwango tofauti- cha chini na cha juu.
Huu ni mwaka wa kwanza, Tanzania inashiriki michuano ya soka ya ufukweni na haina Ligi ya maana tayari ya kuzalisha wachezaji- maana yake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linahitaji kuwekeza zaidi katika mchezo huo kama linahtaji matokeo mazuri.
Katika Raundi ya Kwanza, Tanzania iliitoa Kenya kwa kuifunga nyumbani na ugenini.

![]() |
Wachezaji wa Misri wakishangilia moja ya mabao yao Escape One jioni ya leo |
![]() |
Ally Rabbi wa Tanzania akimtoka Mohammed Faway wa Misri jioni ya leo Escape One |
![]() |
Kocha wa Tanzania, John Mwansasu (kushoto) akiwa mnyonge wakati timu yake inabugizwa mabao na Misri |
Robo ya tatu jahazi la Tanzania inayofundishwa na beki wa zamani wa kimataifa nchini, John Jacob Mwansasu aliyewika Yanga SC, lilizidi kuzama baada ya kumaliza ikiwa nyuma kwa mabao 4-2.
Katika Robo ya mwisho ndipo Tanzania ilitota kabisa na kuongezwa mabao mengine mawili, hivyo kulala 6-2.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi na Mwalimu Akida, wakati mabao ya Misri yalifungwa na Islam Ahmed, Yahia Ally manne na Mohammed Faway.
Kwa ujumla, Tanzania ilizidiwa na Misri na ilionekana dhahiri zimekutana timu mbili za viwango tofauti- cha chini na cha juu.
Huu ni mwaka wa kwanza, Tanzania inashiriki michuano ya soka ya ufukweni na haina Ligi ya maana tayari ya kuzalisha wachezaji- maana yake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linahitaji kuwekeza zaidi katika mchezo huo kama linahtaji matokeo mazuri.
Katika Raundi ya Kwanza, Tanzania iliitoa Kenya kwa kuifunga nyumbani na ugenini.
0 comments:
Post a Comment