// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YAWASILI MWANZA TAYARI KUNOA MAKALI KWA MALAWI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YAWASILI MWANZA TAYARI KUNOA MAKALI KWA MALAWI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 24, 2015

    TAIFA STARS YAWASILI MWANZA TAYARI KUNOA MAKALI KWA MALAWI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM 
    TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama leo asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames), mechi itakayochezwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
    Kikosi cha Stars kimeondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini Mwanza.
    Mbwana Samatta kulia na Thomas Ulimwengu kushoto wa TP Mazembe, tayari wapo Mwanza kuitumikia Taifa Stars

    Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM), Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
    Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).
    Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAWASILI MWANZA TAYARI KUNOA MAKALI KWA MALAWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top