// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STAND UNITED YAICHAPA 1-0 MARA MBILI KAGERA SUGAR, MFUNGAJI YULE YULE MINGERIA KIBOKO YA SIMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STAND UNITED YAICHAPA 1-0 MARA MBILI KAGERA SUGAR, MFUNGAJI YULE YULE MINGERIA KIBOKO YA SIMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 01, 2015

    STAND UNITED YAICHAPA 1-0 MARA MBILI KAGERA SUGAR, MFUNGAJI YULE YULE MINGERIA KIBOKO YA SIMBA

    BAO pekee la Mnigeria Absalom Chidiebele dakika ya 85 limeipa ushindi wa 1-0 Stand United katika mchezo uliochezwa kwa dakika 10 asubuhi ya leo Uwanja wa Kambarage Shinyanga dhidi ya Kagera Sugar.
    Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulianza jana na Stand United ikapata bao moja lililofungwa Chidiebele dakika ya 42. Chidiebele pia ndiye aliyeifungia Stand bao pekee ikiilaza Simba 1-0 wiki iliyopita.

    Hata hivyo, mchezo ulisitishwa zikiwa zimebaki dakika 10 kutokana mvua kubwa kunyeshwa na kuharibu mandhari ya Uwanja, hivyo kumaliziwa leo na Stand kuvuna bao linguine moja hivyo kufanya ushindi wa jumla wa 2-0.
    Kwa matokeo hayo, Stand inatimiza pointi 21 baada ya kucheza mechi 17 na kusogea nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiiteremsha Mtibwa Sugar nafasi ya nane.
    Kagera inabaki na pointi zake 24 katika nafasi ya tatu, nyuma ya Azam Fc pointi 27 na Yanga SC 31.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED YAICHAPA 1-0 MARA MBILI KAGERA SUGAR, MFUNGAJI YULE YULE MINGERIA KIBOKO YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top