// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC INAPOTEA TENA, NA RAIS AMEKWISHAMUWEKEA MKWARA KOCHA, MBONA KAZI IPO MSIMBAZI! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC INAPOTEA TENA, NA RAIS AMEKWISHAMUWEKEA MKWARA KOCHA, MBONA KAZI IPO MSIMBAZI! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 22, 2015

    SIMBA SC INAPOTEA TENA, NA RAIS AMEKWISHAMUWEKEA MKWARA KOCHA, MBONA KAZI IPO MSIMBAZI!

    YANGA SC wapo kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zao 37, baada ya kucheza mechi 18.
    Azam FC, mabingwa watetezi ni wa pili kwa pointi zao 33, baada ya kucheza mechi 17- wanacheza mechi ya 18 leo dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Simba SC ni ya tatu kwa pointi zake 29, baada ya kucheza mechi 19 na leo wanacheza mechi 20 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika Ligi ya timu 14, maana yake Simba baada ya mchezo wa leo, itakuwa imebakiza mechi sita, wakati wapinzani Yanga SC na Azam watakuwa na mechi mbili zaidi.

    Kama Simba SC itashinda mechi zote zilizobaki (saba) itajiongezea pointi 21 na kumaliza na jumla ya pointi 50. 
    Katika mechi nane ambazo kila timu kati ya Azam na Yanga SC watabakiza baada ya michezo ya leo, watahitaji kushinda mechi tano kuifutia kabisa matumaini Simba ya kucheza michuano ya Afrika mwakani. 
    Wakati hali ni hiyo, tayari Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amekwishatoa angalizo kwa benchi la Ufundi la klabu hiyo.
    Aveva amekaririwa akisema; Moja ya mikakati waliyojiwekea ni kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyobakia kwa kutoa maagizo katika benchi la ufundi kuhakikisha agizo hilo linatekelezeka.
    “Kwa sasa hatutazami suala la ubingwa wa ligi msimu huu ila tunachotaka ni kuweza kushinda michezo yetu yote iliyobakia na tayari nimeshatoa maagizo katika benchi la ufundi kwa ajili ya utekelezaji,”.
    “Tunahitaji kumaliza katika nafasi nzuri, hivyo ni lazima tufanye vyema katika mechi zilizobakia bila kupoteza,” amekaririwa Aveva.
    Hapa Aveva hajasema iwapo timu haitashinda mechi zote zilizobaki atachukua gani, lakini msistizo ni kwamba maagizo yake anataka yatekelezeke. Yasipotekelezeka?
    Kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic aliifikisha Simba SC Fainali ya Kombe la Mapinduzi na akaifunga Yanga, lakini akafukuzwa baadaye.  
    Kocha Mzambia, Patrick Phiri naye aliifunga Yanga SC, lakini akafukuzwa.
    Kocha wa sasa, Mserbia Goran Kopunovic ameipa timu Kombe la Mapinduzi na ameifunga Yanga SC, lakini timu inaelekea kukosa nafasi nzuri ambayo Aveva anaitaka.
    Nini mustakabali wake?
    Imekuwa staili ya Simba SC kufukuza makocha baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu- lakini hakuna hakika kama uongozi unachukua hatua sahihi.
    Nasema hatua sahihi kwa sababu, hakuna uhakika kwamba kufanya vibaya kwa timu ni kwa sababu ya makocha.
    SImba SC imekuwa na maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC na wamekuwa wakifanya vizuri katika mechi hizo.
    Wakati fulani timu ilipelekwa kambini Afrika Kusini kwa ajili ya mechi na Yanga SC. Hiyo inaonyesha ni kiasi gani Simba SC wanapenda kufanya vizuri dhidi ya watani wao.
    Lakini timu inaelekea katika mwaka wa tatu bila kucheza michuano ya Afrika na inaelekea staili ile ile ya ‘timua timua’ makocha itaendelea kuchukua nafasi baada ya Simba SC kukosa nafasi nzuri.    
    Ingekuwa vyema, viongozi wa Simba SC wakawa watu wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi- lakini si hivyo, wao wameona kufukuza wachezaji na makocha ndiyo suluhisho, ingawa hatuwaoni kuvuna matunda yake.
    Simba SC inahitaji kutulia na kocha mmoja kwa muda fulani, kutulia na wachezaji wake kwa muda fulani waendelee kuwa pamoja, ili kuzoeana zaidi na hatimaye kuwa na timu imara ya kumudu mikiki ya msimu.
    Lakini kama wataendelea na desturi yao ya kubadili wachezaji na makocha kila wakati wa dirisha la usajili, basi mambo yatabakia kuwa vile vile. Yanga watamfunga. Na Kombe la Mapinduzi watachukua, lakini Ligi Kuu watasubiri sana. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC INAPOTEA TENA, NA RAIS AMEKWISHAMUWEKEA MKWARA KOCHA, MBONA KAZI IPO MSIMBAZI! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top