GWIJI wa Manchester United, Peter Schmeichel ameitaka klabu yake ya zamani kumsajili mshambuliaji PSG, Zlatan Ibrahimovic msimu huu.
Straika huyo mrefu wa kimataifa wa Sweden mara kadhaa amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kabla ya kuchukuliwa na 'vimwaga fedha' wa Ligue 1.
Schmeichel, ambaye alishinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England na moja la Ligi ya Mabingwa wakati wake akicheza United, anaamini Ibrahimovic ana 'mavituz' sawa na magwiji wa zamani wa klabu hiyo, Eric Cantona na David Beckham.
Zlatan Ibrahimovic 'amekaa kaak' kuchezea Manchester United, amesema Peter Schmeichel
Magwiji wa Eric Cantona (kushoto) na David Beckham waling'ara enzi zao Man United
Kipa huyo namba moja wa zamani wa Denmark amesema akizungumza na jarida la L'Equipe: "Anachokifanya PSG ni babu kubwa. Anaipa hadhi na mafanikio makubwa PSG .. Huyu ni mtu ambaye anatekekeza majukumu yake,".
"Msimu uliopita kulikuwa kuna tetesi kwamba angekuja Manchester United. Kisha nikasema kwamba Zlatan aliumbwa kwa ajili ya kucheza huko. Ndiyo maana Cantona alikuwa ana nguvu sana wakati anacheza huko, siyo alipokuwa Leeds au klabu nyingine Ufaransa, kwa nini? Kwa sababu ni Manchester United. Kwa Manchester, wachezaji walikuwa wanapewa uhuru, lakini pia majukumu,"amesema.
0 comments:
Post a Comment