NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa sasa anashika nafasi ya 29 katika orodha ya washambuliaji bora wa ligi tano kubwa Ulaya wakati nyota wa Barcelona, Lionel Messi anashika nafasi ya kwanza.
Shirika la CIES Football Observatory limeorodhesha wachezaji wachezaji bora katika vipengele vitano mwaka huu, likitukia vigezo vya kitaalamu kama kupiga mashuti, kutengeneza nafasi, kuwatoka wapinzani, kusumbua na makali yao uwanjani kwa ujumla.
Katika chati hizo, ajabu Gael Clichy wa Manchester City ametajwa beki bora kulia na Mesut Ozil wa Arsenal ameshika namba katika nafasi ya kiungo mshambuliaji kwa pamoja na Eden Hazard wa Chelsea.
Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya 29 katika orodha ya washambuliaji bora kutoka ligi tano Ulaya mwaka 2015
Ronaldo amefunga mabao sita tu katika La Liga mwaka huu tangu ashinde Ballon d'Or katikati ya Januari, na mpinza ni wake, Messi amempiku mshambuliaji huyo wa Real Madrid kwa mabao yake 19 huku Barcelona ikiongoza Ligi kwa pointi nne zaidi.
Messi, akiongoza orodha hiyo kwa pointi 100 anafuatiwa na mchezaji wa Bayern Munich, Arjen Robben (92), Bas Dost wa Wolfsburg (77) na Luis Suarez wa Barcelona (71).
Nyota wa Barcelona, Messi anaongoza kwa mujbu wa CIES Football Observatory
Gael Clichy (kushoto), pichani katika mechi ya Liverpool All-Star, ndiye beki bora wa pembeni, wakati Marcelo ni wa pili
0 comments:
Post a Comment