• HABARI MPYA

        Sunday, March 22, 2015

        REMY ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA CHELSEA BAO LA USHINDI IKIILAZA 3-2 HULL CITY

        CHELSEA imezidi kupaa kuelekea kwenye ‘ndoo’ ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 3-2 leo dhidi ya wenyeji, Hull City Uwanja wa Kingston Communications.
        Chelsea sasa inatimiza pointi 67 baada ya kucheza mechi 29, ikiwazidi kwa pointi sita mabingwa watetezi, Manchester City.
        Eden Hazard alianza kuifungia Chelsea dakika ya pili kabla ya Diego Costa kufunga la pili dakika ya tisa. Hull walizinduka na kusawazisha mabao yote kupitia kwa Ahmed Elmohamady dakika ya 26 na Abel Hernandez sekunde 74 baadaye.
        Shukrani kwake Loic Remy aliyetokea benchi na kuifungia Chelsea bao la ushindi zikiwa zimebaki dakika 13 mchezo kumalizika. 
        Loic Remy akishangilia na mchezaji mwenzake, Oscar baada ya kuifungia The Blues bao la ushindi

        PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3006614/Hull-City-2-3-Chelsea-Loic-Remy-comes-bench-net-winner-Jose-Mourinho-s-extend-lead-Premier-League.html#ixzz3V8homqn5 

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: REMY ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA CHELSEA BAO LA USHINDI IKIILAZA 3-2 HULL CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry