KIPA wa Bayern Munich, Pepe Reina amemtaka David de Gea kubaki Manchester United, licha ya kwamba anatakiwa na Real Madrid na kusema kwamba ni mmoja wa makipa wakubwa Ulaya.
De Gea, aliyehamia Old Trafford mwaka 2012 akitokea Atletico Madrid, awali alikutana na wakari mgumu kuzoea maisha ya soka ya England, lakini kwa sasa amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kocha Louis van Gaal.
Kiwango chake kwa misimu miwili iliyopita, akiokoa michomo mingi ya hatari kimeivutia Real Madrid ambayo inataka kumchukua akarithi mikoba ya Iker Casillas.
David De Gea amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid anakotakiwa akarithi mikoba ya Iker Casillas
Lakini nyota wa zamani wa Liverpool, Reina, ambaye amekuwa akisotea namba Ujerumani, amesema Gea anapaswa kubaki Manchester licha ya kutakiwa kurudi nyumbani.
"Ni mmoja wa makipa wakubwa Ulaya na mwaka huu amekuwa babu kubwa,' amesema Reina said akizungumza na talkSPORT.
"Labda Real Madrid wanatafuta kipa na De Gea ni moja ya majina yaliyopendekezwa, lakini anapaswa kufurahia kiasi cha kutosha Man United,"amesema.
0 comments:
Post a Comment