Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imepata msaada mkubwa wa taarifa za wapinzani wao katika kampeni ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa kupata siri nzito juu ya klabu ya Platinum ya Zimbabwe.
Yanga ambayo jana ilirejea nchini ikitokea Botswana ilikokwenda kuwatupa nje ya mashindano BDF ya huko wakiwa njiani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta viongozi wao walikutana na Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa ambaye timu yake ilifungwa 4-2 na Platinum.
Mabosi wa Yanga wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro, Katibu wa timu hiyo Dk. Jonas Tibohora na kocha wao Hans Pluijm wametakiwa kuwa makini na Plutinum hasa katika mipira ya faulo,krosi na kona kufuatia Wazimbawe hao kuwa wazuri kwa vichwa.
Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa Yanga SC Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jana
Kalekwa amewaambia Yanga Plutinum ambao wachezaji wao wengi ni warefu kwa maumbo pia wako vizuri katika viungo wa pembeni akiwataka Yanga kuwaanda vyema mabeki wao wa pembeni.
"Jichungeni sana na mipira ya juu mkizubaa wanawafunga lakini pia jiangalieni sana na mawinga wao ni hatari wanachezeshwa na kiungo mmoja ana rasta,"amesema Kalekwa
"Msifanye makosa kama tuliyofanya sisi hakikisheni mnawamaliza nyumbani kwenu kwao hawa ni hatari sana wana fedha za kutosha mkienda kule hakikisheni mnawatuma watu mapema kabla ya timu haijakwenda.

0 comments:
Post a Comment