MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid watamenyana na wapinzani wao wa Jiji, Atletico Madrid - timu ambayo waliifunga katika fainali ya michuano hiyo msimu uliopita.
Los Blancos ilihitaji dakika za nyongeza kuifunga timu ya kocha Diego Simeone mjini Lisbon mwezi Mei, lakini timu hizo mbili za Madrid zitakutana tena katika Robo Fainali mwezi ujao, kuwania tiketi ya kwenda Berlin, Ujerumani.
Kikosi cha Carlo Ancelotti kimeifunga Schalke ili kuingia Robo Fainali, wakati Atletico ilihitaji mikwaju ya penalti kuitoa Bayer Leverkusen Uwanja wa Vicente Calderon Jumanne.
Wakali watatu wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema wanatarajiwa kutetea ubingwa
Droo ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa baada ya kupangwa leo mjini Nyon, Uswisi
0 comments:
Post a Comment