MANCHESTER City imeibamiza mabao 3-0 West Brom Uwanja wa Etihad jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Refa Neil Swarbrick alimuonyesha kadi nyekundu McAuley baada ya sekunde 89, ingawa mtu wa mwisho, Craig Dawson ndiye alistahili kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Wilfried Bony akiwa anakwenda kufunga.
Ikicheza na wapinzani pungufu kwa dakika 88, City ilishinda kiulaini kwa mabao ya Bony dakika ya 27, Fernando dakika ya 40 na David Silva dakika ya 77.
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Bony amefunga bao lake la kwanza leo tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 28 kutoka Swansea City.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Clichy, Jesus Navas, Fernando, Lampard/Jovetic dk65, Silva/Milner dk81, Bony/Dzeko dk78 na Aguero.
West Bromwich Albion; Myhill, Dawson, McAuley, Lescott, Olsson, Baird, Sessegnon/Mulumbu dk89, Fletcher, Gardner, Morrison na Berahino/Anichebe dk86.
Bony akienda chini baada ya kuchezewa rafu na McAuley
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3005457/Manchester-City-3-0-West-Brom-Referee-Neil-Swarbrick-mistaken-identity-storm.html#ixzz3V2InSOB9
0 comments:
Post a Comment