Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TF, Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).
Katika salam zake Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo huo wa awali, umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.
Aidha Rais amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata, bali wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili waweze kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Mchezo wa marduiano unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la Wanawake (All Africa Games Women) zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18 mwaka huu.
Twiga Stars inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa pongezi Twiga Stars kwa ushindi walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.
Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo) yalifungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).

Nahodha Sophia Mwasikili aliifungia bao Twiga Zambia |

0 comments:
Post a Comment