// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAJERUHI KKBAO YANGA IKIWAKABILI WAJESHI LIGI KUU LEO TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAJERUHI KKBAO YANGA IKIWAKABILI WAJESHI LIGI KUU LEO TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 25, 2015

    MAJERUHI KKBAO YANGA IKIWAKABILI WAJESHI LIGI KUU LEO TAIFA

    Kpah Sherman ni majeruhi
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC inashuka dimbani leo kumenyana na JKT Ruvu ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku ikikabiliwa na majeruhi kibao.
    Pamoja na majeruhi, Yanga itawakosa wachezaji wengine kwa sababu ya adhabu za kadi- maana yake makocha Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa wataumiza vichwa kupanga kikosi.
    Mshambuliaji Amisi Tambwe atakuwa nje kwa sababu ya kadi tatu za njano, wakati beki Kevin Yondan, viungo Said Juma Makapu ‘Kizota’, Mrisho Ngassa, Andrey Coutinho na mshambuliaji Kpah Sherman wote ni majeruhi.  
    Lakini habari njema tu ni kwamba, mshambuliaji Dan Mrwanda amemaliza matatizo ya kifamilia na amekuwa kambini na wenzake tangu wiki iliyopita.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC na AFC ya Arusha, alikuwa ana udhuru wa kushughulikia masuala ya kifamilia wiki mbili zilizopita, lakini amerudi kundini na leo anatarajiwa kuanza pamoja na Simon Msuva na Hussein Javu au Jerry Tegete.
    Yanga SC itahitaji ushindi katika mchezo huo, ili kuzidi kupiga kasi katika marathoni ya ubingwa wa Ligi Kuu.
    Hadi sasa, ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 18, Yanga SC ipo kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36 za mechi 18 pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAJERUHI KKBAO YANGA IKIWAKABILI WAJESHI LIGI KUU LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top