• HABARI MPYA

    Friday, March 13, 2015

    MAHAKAMA NAYO YAIGEUKIA SHIRIKISHO KENYA

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    LICHA ya kusitisha kampuni ya ligi kuu Kenya, KPL, kutoendelea na mechi za ligi kuu kufuatia amri yaMahakama, Shirikisho la Soka Kenya, FKF, limepigwa na butwaa baada ya mahakama yiyo hiyo kuligeuka na badala yake kufutilia mbali mashtaka waliyowekea KPL kwa kukiuka orodha ya mahakama.
    KPL ilipuuza amri ya mahakama ilioagiza kutoanza kwa ligi kuu msimu 2015 kwenye barua yao ya tarehe 20 Februari lakini bodi hiyo ikaziamuri timu kucheza mechi za ufunguzi wikiendi ya tarehe 21 na 22 Februari wakisingizia kutoiwahi barua hiyo kwa wakati swala ambalo mahakama kupitia hakimu mkuu wa Mahakama ya Milimani, Nairobi, Roselyn Aburili imebaini kuwa kweli kwenye uamuzi wake mapema Ijumaa tarehe 13 Machi.

    Mashabiki walimiminika Mahakama ya Milimani kusikiza kesi ya leo

    Hatua hiyo ilipelekea Aburili kushusha kesi hiyo kwani FKF hawakuunganisha sababu mwafaka mbona wadau wa KPL wamenyane na minyororo ya sheria.
    Kwa mujibu wa Aburili, FKF waliwapa KPL nakala hiyo kuchelewa na masaa machache tu ligi kung’oa nanga lakini pindi tu KPL walipotia sahihi kwenye nakala hiyo siku tatu baadaye, walisonga mbele na kusimamisha ligi hiyo hadi kesi hiyo itakaposikizwa.
    Iwapo wangepatikana na makosa, wadau wa KPL yaani katibu mkuu mtendaji Jack Oguda, wenyekiti Ambrose Rachier (Gor Mahia), Allan Kasavuli (AFC Leopards), Juma Mwinyikali (Ulinzi Stars), Muingereza Ellio Loli (Thika United), Mkongo Elly Kalekwa (Sofapaka), James Musyoki (Tusker FC) na Mkanada Bob Munro (Mathare United) wangehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani.
    Mahakama pia ilimtuhumu rais wa Shirikisho Sam Nyamweya kupitia kwa wakili wake Eric Mutua kwa kudanganya korti kuwa alimpigia simu Oguda ijumaa 20 Februari akimwagiza kusitisha ligi kuu kwani wao si wanachama wa FKF ambalo ni shirikisho lililoidhinishwa na FIFA, CAF na CECAFA kuendeza shughli zozote za kandanda nchini.
    Kwa hayo, Aburili aliagiza pande zote mbili kubeba misalaba yao huku akifichua kuwa kesi ya kwanza kuhusu kusitishwa kwa ligi kuu itasikizwa siku ya Jumatatu tarehe 16 Machi.
    Hiyo ndiyo siku wakenya watabaini iwapo kutakuwa na ligi ya KPL ama ile mbadala ya FKF itazidi kutawala kwani kufikia sasa hivi mechi zake zimeweza kusakatwa huku ligi ya KPL ikiwa imekwama.
    Mivutano hii yote ni kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki ligi kuu Kenya msimu huu  na ni nani atasimamia shughli hiyo; FKF wanataka timu ziwe18 huku wasimamizi wa ligi, KPL wakizitaka zisalia 16 ilivyokuwa tangu mwaka 2003.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAHAKAMA NAYO YAIGEUKIA SHIRIKISHO KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top