MECHI mbili kubwa Ulaya zinafanyika Jumapili, kwanza mahasimu wa jadi wa England na baadaye wapinzani wa jadi wa Hispania.
Liverpool itakuwa mwenyeji wa Manchester United Uwanja wa Anfield kuanzia Saa 7.30, na baadaye Real Madrid watakwenda Uwanja wa Nou Camp kumenyana na Barcelona Saa 2:00 usiku.
Safari ya United kwa Liverpool itakuwa ya kuwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, wakati El Clasico itakuwa mechi ya kuwania ubingwa wa La Liga.
Kwa matokeo yoyote, klabu hizo nne zinabaki kuwa za kihistoria katika nchi zao. Lakini nani ni zaidi ya mwenzake kw amafanikio na hata kutumia fedha nyingi kujenga timu?
Luis Suarez akijaribu kuwatoka Karim Benzema (kushoto) na Sergio Ramos katika Clasico ya Oktoba
Beki wa Liverpool, Kolo Toure akipambana na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney timu hizo zilipokutana mara ya mwisho
MECHI KUBWA ENGLAND vs MECHI KUBWA HISPANIA
Zitakavyotazamwa kwenye TV duniani
Mechi hizo zote mbili zitatazamwa na watu wa dunia nzima kupitia Televisheni. Ligi Kuu ya England ni maarufu zaidi, ikiwa inakadiriwa kutazamwa na watu zaidi ya Milioni 700 - lakini pia inaonyeshwa karibu mara nne katika nchi nyingi.
Liverpool vs Manchester United (El Vitriol): Watu kati ya Milioni 600 hadi 700 wataitazama
Barcelona vs Real Madrid (El Clasico): Watu kati ya Milioni 400 na 500 wataitazama
nchi zitakazoonyesha;
El Vitriol 212 v 56 El Clasico
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiburu kamera ya televisheni msimu uliopita Old Trafford
Nyota wa Real, Cristiano Ronaldo na Barcelona, Lionel Messi wanavutia zaidi watazamaji wa TV duniani kote
Pato la mwaka (msimu wa 2013/2014)
Timu zote nne zipo kwenye 10 bora ya klabu tajiri Ulaya, baada ya takwimu za mara ya mwisho, huku Real Madrid ikiwa inaongoza, kwa kuwa na utajiri wa Pauni Milioni 459.5 mbele ya Manchester United.
Orodha iko hivi; Real Madrid: Pauni Milioni 459.5, Manchester United: Pauni Milioni 433.2, Barcelona Pauni Milioni 405.2, Liverpool Pauni Milioni 255.8, El Vitriol Pauni Milioni 689 v Pauni Milioni 864.7 El Clasico
Pato la Real Madrid liliwaruhusu kumsajili Gareth Bale kwa Pauni Milioni 85
Manchester United walivunja rekodi yao ya usajili kwa kumnunua Angel di Maria kwa Pauni Milioni 60
Mauzo ya jezi (wastani kwa mwaka)
Hapa, Real na United 'zinakula sahani moja', zote zikiuza hadi jezi Milioni 1.5 kila mwaka.
Real Madrid: Milioni 1.2 – Milioni 1.5
Manchester United: Milioni 1.2 – Milioni 1.5
Barcelona: Milioni 1 – Milioni 1.2
Liverpool: 700,000 – 900,000
El Vitriol Milioni 2.4 v Milioni 2.7 El Clasico
Mashabiki wa Liverpool wakiwa wamependeza na jezi za timu zao katika mechi ya kujiandaa na msimu kwenye ziara ya Melbourne
Wafuasi wa Twitter
Klabu hizo mbili za Hispania zinaziacha mbali klabu za England kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii. Na ni Real ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wafuasi 800,000 zaidi kwenye tweeter.
Real Madrid: Milioni 15.2
Barcelona: Milioni 14.4
Manchester United: Milioni 4.63
Liverpool: Milioni 4.07
El Vitriol Milioni 8.7 v Milioni 29.6 El Clasico
Real Madrid inaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye Twitter
Wachezaji wa gharama kikosi cha kwanza
Baada ya kupitia ada za uhamisho za vikosi vyote vya kwanza vya timu zote nne, Real inakuwa juu kwa zaidi ya pauni Milioni 100 ikiwa ina kikosi cha thamani ya Pauni Milioni 364. Usajili wa kufuru wa United msimu huu, unawabeba hadi nafasi ya pili juu ya Barcelona.
Real Madrid: Pauni Milioni 364
Manchester United: Pauni Milioni 255.6
Barcelona: Pauni Milioni 251.8
Liverpool: Pauni Milioni 175.5
El Vitriol Pauni Milioni 431.1 v Pauni Milioni 515.8 El Clasico
Cristiano Ronaldo ndiye nyota mwenye mvuto zaidi Real Madrid kwa sasa
Lionel Messi na Neymar ndiyo nyota wenye mvuto zaidi Barcelona kwa sasa
Nyota wa kiwango cha dunia
Vigezo vinavyotazamwa hapa ni uwezo wa mchezaji, kutajwa katika kuwania tuzo mbalimbali, kushinda mataji, kucheza Kombe la Dunia na ada za uhamisho.
Barcelona: Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar, Xavi na Andres Iniesta.
Real Madrid: Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, James Rodriguez na Toni Kroos.
Manchester United: Wayne Rooney, Angel di Maria na Radamel Falcao.
Liverpool: Hakuna (Raheem Sterling anaweza baadaye)
El Vitriol 3 v 9 El Clasico
Liverpool inatunai siku moja Raheem Sterling atakuwa mchezaji wa kiwango cha dunia
Wayne Rooney ndiye Nahodha wa Manchester United na mmoja wa nyota wao wenye mvuto
Mataji makubwa
Real Madrid: Mataji 32 ya La Liga, 10 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya UEFA, 19 ya Copa del Rey (Jumla 63)
Barcelona: Mataji 22 ya La Liga, manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, manne ya Kombe la Washindi la UEFA, 26 ya Copa del Rey (Jumla 56)
Liverpool: Mataji 18 ya Ligi Kuu, matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, matatu ya Kombe la UEFA, saba ya FA, nane ya Kombe la Ligi (Jumla 41)
Manchester United: Mataji 20 ya Ligi Kuu, matatu ya Ligi ya Mabingwa, moja la Kombe la Washindi la UEFA, 11 ya FA, manne ya Kombe la Ligi (Jumla 39)
El Vitriol 80 v 119 El Clasico
Real Madrid wakiinua Kombe la 10 la Ligi ya mabingwa baada ya kuifunga Atletico mjini Lisbon Mei mwaka jana
Liverpool walishinda taji la tano la Ligi ya Mabingwa mjini Istanbul muongo mmona uliopita
Manchester United walishinda taji la pili kati ya matatu ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga Bayern Munich mjini Barcelona mwaka 1999
Wachezaji wa Barcelona wakisherehekea taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya walilotwaa mara ya mwisho mwaka 2011 kwa kuifunga Man United chini ya kocha Pep Guardiola
Ukubwa wa viwanja
Timu zote nne zina viwanja babu kubwa na vya kisasa. Uwanja wa Nou Camp wa Barcelona ndiyo mkubwa zaidi ukiwa unameza mashabiki wapatao 100,000.
Nou Camp: 99,354
Bernabeu: 85,454
Old Trafford: 75,811
Anfield: 45,522
El Vitriol 121,333 v 184, 808 El Clasico
0 comments:
Post a Comment