// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIUNGO YANGA ALIZIMIA UWANJANI LEO BAADA YA PIGO LA MCHEZAJI WA MGAMBO, ILA SASA YUKO POA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIUNGO YANGA ALIZIMIA UWANJANI LEO BAADA YA PIGO LA MCHEZAJI WA MGAMBO, ILA SASA YUKO POA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 22, 2015

    KIUNGO YANGA ALIZIMIA UWANJANI LEO BAADA YA PIGO LA MCHEZAJI WA MGAMBO, ILA SASA YUKO POA

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    YANGA SC ilimaliza pungufu mechi ya leo dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting, baada ya kiungo wake chipukizi, Said Juma ‘Kizota’ kuumia zikiwa zimesalia dakika nne na kukimbizwa hospitali.
    Wakati huo, tayari vinara hao wa Ligi Kuu walikuwa wamekwishamaliza idadi ya wachezaji wa kubadili- na wakalazimika kucheza tisa, bahati nzuri wakaulinda ushindi wao wa 2-0.
    Imeelezwa Said alipoteza fahamu baada ya kuumia na kukimbizwa hospitali ya Bombo, ambako hata hivyo baadaye alipata ahueni na kurejeshwa kambini.
    Said Juma 'Kizota' kulia alizimia leo dhidi ya Mgambo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba kiungo huyo anaendelea vizuri.
    “Alipata pigo chini ya kifua, akaanguka na kutolewa nje kwa machela, lakini ikagundulika amepoteza fahamu akakimbizwa hospitali, ila kwa sasa anaendelea vizuri tunamshukuru Mungu,”alisema Muro.
    Kikosi cha Yanga SC inaondoka kesho asubuhi mjini hapa kuerejea Dar es Salaam ambako Jumatano kitakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Ruvu.
    Baada ya mechi na JKT Ruvu, Yanga SC itasafiri kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Platinum FC, wakijivunia mtaji wa ushindi wa 5-1 katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO YANGA ALIZIMIA UWANJANI LEO BAADA YA PIGO LA MCHEZAJI WA MGAMBO, ILA SASA YUKO POA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top