MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amekuwa akibubujikwa machozi anapofikiria mustakabali wake katika klabu ya Manchester United, amesema wakala wa zamani wa mchezaji huyo wa Colombia.
Silvano Espindola amesema kwamba Falcao alimpigia simu kutoka Old Trafford wiki iliyopita alipopelekwa katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 akacheze dhidi ya Tottenham na akasema ameumizwa sana na hali hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 pia alimwaga machozi akisema kwamba anahatarisha goti lake lenye maumivu kuchezeshwa dhidi ya wapinzani vijana wa kiwango cha chini.
Falcao alipangwa katika kikosi cha vijana cha United kucheza dhidi ya Tottenham, lakini akashindwa kung'ara katika mchezo huo
Falcao analipwa Pauni 280,000 kwa wiki katika mkataba wake wa mkopo United kutoka Monaco, lakini inaonekana kama mpango wa Louis van Gaal kumnunua jumla kwa dau la Pauni Milioni 43 mwishoni mwa msimu unaweza kufa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Porto na Atletico Madrid amefunga mabao manne tu na hajaanzishwa katika kikosi cha kwanza cha United kwa wiki tatu sasa.
Espindola, rafiki wa karibu wa Falcao na mwakilishi wake wa zamani, amesema; "Tulizungumza sana. Siwezi kukuambia anajisikia furaha, kwa sababu hajisikii hivyo. Tunazungumza mara nyingi, na tunalia pamoja,".
Silvano Espindola (kushoto), wakala wa zamani wa Falcao, ameelezea namna nyota huyo wa Colombian asivyofurahia maisha Man United
0 comments:
Post a Comment