Mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Colombia ikiichapa 6-0 Bahrain katika mchezo wa kirafiki usiku huu. Falcao, ambaye hafanyi vizuri Man United anapocheza kwa mkopo kutoka Monaco ya Ufaransa, sasa amefikisha mabao 23 aliyoifungia Colombia katika mechi 55. Mabao mengine ya Colombia yamefungwa na Carlos Bacca, Adrian Ramos, Johan Mojica na Andres Renteria. Mara ya mwisho Falcao aliifungia Manchester United Januari 31.
Mshambuliaji wa Manchester United akifunga bao lake la kwanza usiku huu
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3013552/Bahrain-0-6-Colombia-Radamel-Falcao-strikes-twice-striker-sends-message-Manchester-United-boss-Louis-van-Gaal.html#ixzz3VX1umYrK
0 comments:
Post a Comment