ENGLAND imeifumua mabao 4-0 Lithuania katika mchezo wa Kundi E Kufuzu Fainali za Mataifa ya Ulaya usiku huu Uwanja wa Wembley, London, England.
Nahodha Wayne Rooney alifunga bao la kwanza dakika ya sita hilo likiwa bao lake la 47 timu ya taifa, kabla ya Danny Welbeck kufunga la pili dakika ya 45.
Raheem Sterling alimalizia krosi ya Rooney kufunga bal tatu dakika ya 58 kabla ya Harry
Kane kuhitimsha ushindi huo kwa bao la dakika ya 71 akiichezea England kwa mara ya kwanza.
Ushindi huo, unaifanya England ifikishe pointi 15 baada ya mechi tano na kuendelea kujinafasi kileleni mwa kundi E, mbele ya Slovenia yenye pointi tisa sawa na Uswisi, wakati Lithuani ina pointi sita.
Kikosi cha England kilikuwa; Hart, Clyne, Cahill, Jones, Baines, Henderson/Barkley dk71, Carrick, Delph, Sterling, Welbeck/Walcott dk76 na Rooney/Kane dk71.
Lithuania; Arlauskis, Freidgeimas, Zaliukas, Kijanskas, Andriuskevicius/Slavickas dk83, Chvedukas, Zulpa, Mikuckis/Stankevicius dk66, Mikoliunas/Kazlauskas dk88, Cernych na Matulevicius.
Rooney na Welbeck wakipongezana kwa kazi nzuri waliyoifanyia England
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3015343/England-4-0-Lithuania-Harry-Kane-scores-79-seconds-coming-Wayne-Rooney-Danny-Welbeck-Raheem-Sterling-seal-rout.html#ixzz3VdMkMoEt
0 comments:
Post a Comment