// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); COUTINHO, CANNAVARO HALI BADO TETE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE COUTINHO, CANNAVARO HALI BADO TETE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Friday, March 13, 2015

    COUTINHO, CANNAVARO HALI BADO TETE

    Andrey Coutinho akiwa nje mazoezi leo
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC itawakosa Nahodha wake, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Mbrazil Andrey Coutinho katika mchezo wa Jumapili dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.
    Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Jumapili watakuwa wenyeji wa Platinum FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza, Raundi ya Kwanza, Kombe la Shirikisho la Soka Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Nahodha Cannavaro hakutokea kabisa mazoezini Uwanja wa Karume asubuhi ya leo, wakati Coutinho pamoja na kufika, lakini hakufanya mazoezi na wenzake.
    Coutinho akiwa na Dk Sufiani mazoezini leo asubuhi

    Mbrazil huyo aliyeumia wiki tatu zilizopita mjini Mbeya akiichezea timu hiyo dhidi ya Prisons mchezo wa Ligi Kuu, alikuwa akifanyishwa mazoezi maalum na Daktari wa Yanga SC, Sufiani Juma.
    Dk Sufiani aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba, Coutinho bado yupo kwenye programu maalum na hataweza kujumuika na wenzake kwa programu kamili ya mazoezi.
    Maana yake, zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya mchezo, Coutinho hawezi kucheza Jumapili kwa sababu hadi leo ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake.
    Kwa upande wake, Cannavaro aliyeumia katika mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC Jumapili, naye hakutokea mazoezini baada ya kushonwa nyuzi tisa juzi kufuatia kuchanika sehemu ya jichoni.
    Wazi, Cannavaro naye hatacheza Jumapili, kwa kuwa hadi leo hajafanya kabisa mazoezi tangu acheze mara ya mwisho dhidi ya Simba SC, Yanga ikilala 1-0.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COUTINHO, CANNAVARO HALI BADO TETE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry