CHELSEA imetwaa taji la Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup usiku huu Uwanja wa Wembley kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham.
Nahodha wa Blues, John Terry aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 45 akimtungua Hugo Lloris, kabla ya Kyle Walker kujifunga baada ya kubabatizwa na shuti la Diego Costa dakika ya 56.
Kocha wa Chelsea, Mreno Jose Mourinho amesherehekea kutwaa taji la kwanza baada ya kurejea kuifundisha timu hiyo.
Kikosi cha Tottenham kilikuwa; Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Rose, Bentaleb, Mason/Lamela dk71, Chadli/Soldado dk80, Eriksen, Townsend/Dembele dk62 na Kane.
Chelsea; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Zouma, Hazard, Fabregas/Oscar 88, Willian/Cuadrado dk76 na Diego Costa/Drogba dk90.
Nahodha wa Chelsea, John Terry akiinua Kombe la Capital One baada ya kuifunga Tottenham 2-0 Uwanja wa Wembley
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2974579/Chelsea-2-0-Tottenham-John-Terry-strike-Kyle-Walker-s-goal-win-Capital-One-Cup.html#ixzz3T9ykRYWe
0 comments:
Post a Comment