// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CAF YAMPIGA STOP STRAIKA MGOMVI WA SIMBA KUCHEZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CAF YAMPIGA STOP STRAIKA MGOMVI WA SIMBA KUCHEZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 31, 2015

    CAF YAMPIGA STOP STRAIKA MGOMVI WA SIMBA KUCHEZA

    Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemzuia mshambuliaji tegemeo wa URA ya Uganda, Robert Ssentongo kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini mwishoni mwa wiki.
    URA inakabiliwa na mtihani wa kukipiku kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza Afrika Kusini bila mkali wao huyo wa mabao, Ssentongo ambaye amewahi kuchezea African Lyon na Simba SC za Dar es Salaam.
    Timu hizo mbili zinakutana katika Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole kwenye mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho, URA wakihitaji ushindi wa 1-0 kusonga mbele Raundi ya Pili.
    Ssentongo kulia wakati akiichezea Simba SC. Mchezaji huyo amezuia kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya timu yake ya sasa, URA dhidi ya Orlando Pirates Jumamosi

    Mfungaji huyo bora wa URA katika michuano hiyo ya Afrika akiwa amefunga mabao matatu kati ya matano ya timu hiyo, Ssentongo, aliyekosa mchezo wa kwanza dhidi ya Pirates nchini Afrika Kusini, pia anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya Uganda, amefunga mara 10.
    Ssentongo atakosekana na Jumamosi pia baada ya kikao cha Kamati ya Nidhamu ya CAF kuamua kwamba, kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa marudiano dhidi ya Elgeco Plus Raundi ya Awali nchini Madagascar ilitokana na kufanya vurugu.
    Kocha wa URA, Alex Isabirye amesema hakuona tukio ambalo lilimponza mshambuliaji huyo akatolewa kwa kadi nyekundu katika mechi hiyo ya Raundi ya Awali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAMPIGA STOP STRAIKA MGOMVI WA SIMBA KUCHEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top