Na Mahmoud Zubeiry, TANGA
BEKI na kiungo wa zamani wa Simba SC, Hassan Banda (pichani kushoto) amesema mwanawe, Abdi Banda anayecheza klabu hiyo ni mtoto wa damu wa klabu hiyo.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Banda mkubwa amesema kwamba kijana wake alizaliwa wakati yeye anachezea Simba SC mwaka 1991.
“Huyu Abdi leo kucheza Simba SC ni historia moja tamu sana. Kwa sababu huyu mtoto alizaliwa wakati mimi nacheza Simba SC. Ilikuwa mwaka 1991, kwa kweli ni faraja sana kwangu,”amesema Hassan Banda.
Aidha, Hassan Banda amesema kwamba anafurahi mno kijana wake huyo kufuata vyema nyayo zake kwa kumudu kucheza vyema nafasi za ulinzi na kiungo.
“Niseme tu ni jitihada zake mwenyewe katika mazoezi zimemfikisha hapa. Na ninaamini Abdi atakuwa mchezaji mkubwa zaidi ya hapa, kwa sababu ana kipaji na juhudi za mazoezi pia,”ameongeza.
Mbali na Abdi, watoto wengine wawili wa kiume wa Hassan wamefuata nyayo za baba yao katika soka, kwani Ally mwenye umri wa miaka 28 pia ni mchezaji mzuri, ingawa hajafanikiwa kuchezea klabu kubwa, hadi sasa akiwa anachezea Bomboka FC ya Tanga na Omar mwenye umri wa miaka 14 anachipukia vizuri katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Coastal Union.
Hassan Banda mwenye umri wa miaka 50 sasa, enzi zake aliwika katika klabu ya African Sports miaka ya 1980 kabla ya kusajiliwa Simba SC mwaka 1990.
Hassan Banda alikuwemo kwenye kikosi cha Simba SC kilichotwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kombe la Kagame mara mbili mfululizo mwaka 1991 mjini Dar es Salaam na 1992 visiwani Zanzibar.
Abdi Banda amesajiliwa Simba SC msimu huu kutoka Coastal Union na sasa ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Wekundu wa Msimbazi, akiwa ana uwezo wa kucheza namba karibu zote za nyuma na kiungo pia, chini na juu.

Abdi Banda kulia amefuata nyayo za baba yake Simba SC |

0 comments:
Post a Comment