Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
MWISHONI mwa wiki, wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga na Azam fc walikuwa na vibarua vipevu vya kupeperusha Bendera ya Taifa la Tanzania. Azam fc walikuwa katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wakati Yanga wapo katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kabla ya Azam haijavaana na El-mereck ya Sudan ,Yanga ilianza kuonyesha njia baada ya kuwazaba wanajeshi kutoka Botswana (BDF) Uwanja wa Taifa Dar es salaam Kwa mabao 2-0. Siku iliyofuta Azam waliwakaribisha El-mereck uwanja wa Chamazi na Azam ikaondoka na ushindi wa Mabao 2-0.
Baada ya wiki mbili timu hizo zilisafiri kwenda kurejeana na timu hizo,Yanga ikaanza kufungwa kwa magoli 2-1 huko Botswana.
Pamoja na Kufungwa Yanga inasonga mbele kwa Jumla ya magoli 3-2. Siku iliyofuata Huko Sudan Azm ikashuka Dimbani kurejeana na El-Merecck timu inayosifika kwa hila bila kuchukuliwa hatua.
Pamoja na Kdhia zote zilizotokea Uwanja na nje ya Uwanja mpaka Dakika 90 zinakamilika El-Merecck ikaondoka na Ushindi wa magoli 3 -0.
Hivyo Azam fc ikaondoshwa kwa Jumla ya Magoli 3-2.
Namkumbuka Mwalimu wangu niliyokuwa namsoma toka nipo shule ya Msingi Unga ltd Arusha. Dk. Gedion Shoo.
Siku moja akaandika hivi.`` Ujuha au uwendawazimu ni hali ya mtu ama watu kufanya jambo lile lile ,wakati uleule na kwa mtindo uleule huku wakitaraji matokeo tofauti.( Mwisho wa kumnukuu)
Alimaanisha ukichaa au uwendawazimu ni hali ya mtu kufanya jambo kwa mtindo uleule na akitarajia matokeo tofauti na siyo lazima atembee bila nguo majiani. Huo unatosha kuwa Uwendawazimu.
Niizungumzie kidogo Yanga iliyosonga mbele `kwa bahati tu`. Kwanza urahibu wa wachezaji wa Tanzania ( Yanga?) kuridhika mapema ama kwa magoli machache au goli moja iliendelea kudhihirika huko Botswana.
Yanga waliingia wakiwa na mtaji wa Magoli 2 waliyoyapata Tanzania. Ingawa walipoanza mchezo hawakuonyesha kujihami bali walishambulia ( lilikuwa jambo jema).
Baada ya Yanga kupata Goli `utamaduni` ukaanza kuonekana kidogo kwa wachezaji kuridhika wasionyeshe njaa zaidi ya kutafuta magoli.
Kipindi Cha pili BDF Waliongeza Nguvu ingawa walipata pigo kwa kuondolewa mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu. Ndipo hapo Mwamuzi akaanza visa vya kutaka kufuta matozi ya wenyeji.
Kweli akampa kadi Nyekundui Danny Mrwanda. Kadi ambayo haikustahili adhabu hiyo hata kama alikuwa tayari ana kadi ya Njano.
Kdiri Muda ulivyosonga mbele Mwamuzi naye alikuwa akibadilika kama Kinyonga na kuwabeba wenyeji. Mungu saidia muda nao ukazidi kuyoyoma na ndiyo ikawa salama ya Yanga.Hivyo basi pamoja na Mwamuzi kuonekana kutokuwa `fear` wachezaji wa Yanga ni Lazima wabadilike kama wanataka kusonga mbele kwa Plutinum ya Zimbabwe hata kama Zimbabwe hawana historia nzuri katika michuano ya kimataifa.
Nirudi kwa Azam fc. Jambo walilofanyiwa Azam fc huko Sudan ni jambo bayasana ingawa si geni katika Nchi hiyo na hata timu hiyo ya El-Mereck.
Kabla ya Kuondoka Tanzania Azam walishafahamu kuwa Timu hiyo inaongoza kwa `fitna` walijua kuwa watakutana na madhila kama hayo ikiwa ni pamoja na `kunyongwa` na mwamuzi na hata nje ya uwanja wakitua tu uwanja wa Ndege.
Ni kweli wakapokewa na Gari lisilokuwa na hadhi,wakakalishwa uwanja Ndege kwasababu za `kipuuzi tu`.
Wakati wa Pambano huko majukwaani risasi ziliendelea kurindima,moto uliwashwa na lugha mbalimbali zisizovikwa nguo zikatolewa dhidi yao. Wakati wa mapumziko uwanja ulikuwa ukimwagiwa maji ( siyo utaratibu)
Mwamuzi Naye akadhihirisha na kuendelea kutoa somo kwa Watanzani juu ya `upuuzi wa upendo wao` ( siyo upendo ni kiherehere)
Ni Dhahiri Mwamuzi aliwabeba wenyeji tena si kidogo.Kuna taarifa yupo Mtu anaitwa Shams el din Raia wa Sudan anayehusika kupanga waamuzi na huwapa maelekezo ya timu ya kushinda.
Huyo Shams, Fifa au CAF Siyo za Mama yake au Babayake na wala haiwerzi kuwa ya Mama yake hata siku moja.( havikubaliki hata kidogo katika michezo)
Ninasema Azam fc wameponzwa na Uwendawazimu kwasababu zifuatazo.
Tulikuwa tunanafasi ya kufanya yote waliyoyafanya El Mereck huko kwao, tena tulikuwa na uwezo wakufanya makubwa kuliko waliyoyafanya wao huko kwao (penye vita vyakijinga)
Tuilikuwa tunajua hawa jamaa kwao si binadamu,tulipaswa kabisa kuwafanyia zaidi ya ubinadamu hapa kwetu. Lakini tumefanya jambo lilelile wakati uleule tukitarajia matokeo tofauti( ni ujuha)
Kama kufanya hayo waliyofanya El mereckk ni kosa mbona hawachukuliwi hatua na siyo mara moja ama mbili!! Kwanini sisi tusifanye?? Wakati mwingine vikundi kama vya boko haramu na wenzao hujitokeza kwa sababu za `kishenzi` kama hizi,haiwezekani upendo wako ukufanye udhalilike kila mwaka na kisha ukaendelea na ukarimu huohuo. Huo ni uwendawazimu na ujuha wakupitiliza, ni umbilikimo wa kufikiria na ujinga . Inaudhi sana…..!!!!
(Mwandishi wa Makala haya ni Mtangazaji wa ITV na Redio One, ambaye anapatikana kwa namba +255 752 250157 na _255 655 250157).

Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akimtoka beki wa El Merreikh katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam |
Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima akimtoka kiungo wa BDF katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam |

0 comments:
Post a Comment