Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC imelalamikia mchezo wake dhidi ya Ndanda FC kupelekwa Jumatatu, wakati Jumamosi na Jumapili hakutakuwa na mchezo wowote Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, waliomba mchezo huo ufanyike Jumamosi, ili kupisha mchezo wa Yanga SC na Platinum Jumapili, lakini ajabu umepelekwa Jumatatu.
Kawemba amesema kwamba hawaelewi dhamira ya Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuupeleka mchezo huo Jumatatu, wakati wikiendi yote Uwanja wa Azam Complex utakuwa mtupu.
Saad Kawemba (kulia) akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Azam FC, Abubakar Bakhresa (kushoto).
“Unajua sasa hivi Ligi Kuu inaelekea ukingoni, inapendeza mechi zote zichezwe kwa wakati mmoja ili kukwepa kupanga matokeo na pia kufanyiana fitina,”.
“Sisi tumeelewa kwamba wenzetu Yanga SC wapo kwenye mechi za Kombe la Shirikisho. Hao kutocheza mechi ya Ligi wikiendi hii ni sawa, lakini kwa nini tusicheze siku moja na Simba SC (Jumamosi)?”amehoji Kawemba.
Mtendaji huyo Mkuu amesistiza kwamba ili kuepuka ‘mchezo mchafu’ ni vyemba mechi za Ligi Kuu zikachezwa kwa wakati mmoja zote wakati ligi hiyo ikiwa imefika ukingoni.
Amesema wamejaribu kuwasiliana na wahusika juu ya hilo, lakini bado majibu si ya kuyaridhisha. “Sisi tunataka kucheza Jumamosi. Na hata kimapato, wikiendi ni siku nzuri watu wanakwenda uwanjani,”amesema Kawemba.
Ameongeza kwamba siku zote mechi zimekuwa zikichezwa Uwanja wa Azam Complex, wakati Uwanja wa Taifa kuna mechi nyingine za Ligi Kuu, hivyo anashangaa sasa hivi ishindikane.
“Mara ngapi sisi au JKT Ruvu tunacheza Chamazi, wakati Uwanja wa Taifa, Simba au Yanga wanacheza?”amehoji.
“Msimu uliopita tumecheza mechi za mwisho za ligi, sisi tunacheza na JKT Ruvu Chamazi, wakati Taifa wanacheza Simba na Yanga, iweje sasa hivi ishindikane?,” ameongeza Kawemba.
Mtendaji huyo Mkuu ameiomba TFF na Bodi ya Ligi watumie busara kuhakikisha hawavurugi Ligi Kuu katika hatua hizi za mwishoni.
Ligi Kuu inaelekea ukingoni, wakati Yanga SC ikiwa inaongoza mbio za ubingwa kwa pointi zake 31 za mechi 16, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 30 za mechi 16 pia na Simba SC pointi 26 za mechi 17.
Simba SC wanatarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Yanga baada ya Jumapili kucheza na Platinum FC ya Zimbabwe katika Kombe la Shirikisho watacheza na JKT Ruvu katikati ya wiki.

0 comments:
Post a Comment