ARSENAL imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St James Park usiku huu.
Olivier Giroud aliunganisha mpira wa kichwa wa Danny Welbeck akimtungua kipa Tim Krul kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 24.
Mfaransa huyo akaifungia timu yake hiyo bao la pili dakika nne baadaye, kabla ya Moussa Sissoko kuifungia Newcastle bao la kufutia machozi dakika ya 48.
Matokeo hayo, yanaifanya Arsenal inaki inazidiwa pointi moja na Manchester City nan ne na vinara Chelsea.
Kikosi cha Newcastle kilikuwa: Krul, Ryan Taylor, Janmaat, Williamson, Colback, Anita/Gutierrez dk72, Sissoko, Gouffran, Cabella, Ameobi/Armstrong dk89 na Perez.
Arsenal: Ospina, Chambers, Gabriel, Koscielny, Monreal, Ramsey, Coquelin, Sanchez/Flamini dk71, Welbeck/Bellerin dk89, Cazorla/Rosicky na Giroud.
Olivier Giroud akishangilia na wenzake Gabriel Paulista na Welbeck (kulia) Uwanja wa St James' Park
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3005555/Newcastle-United-1-2-Arsenal-Olivier-Giroud-scores-twice-Gunners-pressure-Manchester-City-Chelsea.html#ixzz3V2ihkg5M
0 comments:
Post a Comment