MUSTAKABALI wa kiungo Mcameroon Alex Song haueleweki kwa sasa baada ya kugundulika klabu ya West Ham inasuasua kumsaini moja kwa moja kwa sababu ya mshahara wake mkubwa.
Song amecheza kwa mkopo msimu wote huu Upton Park kutoka Barcelona, lakini kushuka kwa kiwango chake mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya England kumemuweka njia panda.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, ambaye ana Mkataba na klabu ya Nou Camp hadi mwaka 2017, analipwa mshahara wa Pauni 80,000 kwa wiki. West Ham, ambayo ilivutiwa na kiwango cha mwanzoni cha mchezaji huyo, inajishauri kumsajili moja kwa moja kutokana na mshahara wake mkubwa.
Alex Song mustakabali wake kwa sasa haueleweki kama atabaki West Ham au atarejeshwa Camp Nou ambako alikuwa hapati nafasi kikosi cha kwanza
0 comments:
Post a Comment