// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); 50 CENT AWEKA DOLA 'MILIONI NA UPUUZI' MAYWEATHER ATAMDUNDA PAQCUIAO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE 50 CENT AWEKA DOLA 'MILIONI NA UPUUZI' MAYWEATHER ATAMDUNDA PAQCUIAO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 04, 2015

    50 CENT AWEKA DOLA 'MILIONI NA UPUUZI' MAYWEATHER ATAMDUNDA PAQCUIAO

    RAPA 50 Cent ametambiria ushindi bindia Floyd Mayweather Jnr katika pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao Mei 2, mwaka huu.
    50 Cent, ambaye aliwahi kuwa katika kambi ya The Money Team, amepanga kuweka dau la dola za Kimarekani 1.6 kumtabiria ushindi Mayweather dhidi ya Pacquiao Mei 2.
    Ikiwa Mayweather ataibuka kinara mjini Las Vegas siku hiyo, basi 50 Cent - ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson atavuna kitita cha dola Milioni 2.3 katika beti yake hiyo.
    The rapper (left), pictured with Mayweather (right) in 2007, would pocket £1.5m Pacquiao is defeated
    50 Cent (kushoto), akiwa na Mayweather (kulia) enzi za urafiki wao mwaka 2007

    "Nimempata bingwa," alisema katika The Breakfast Club. "Bingwa atamtandika yeye. Itaonekana kama hakukuwa na sababu ya pambano hilo,".
    50 Cent alisema alimfuata Mayweather katika onyesho la Chris Brown ukumbi wa Barclays Centre mjini New York na hicho ndicho alichokuwa anafikiria.
    Ilikuwa ni mwaka jana tu wakati wawili hao walipokuwa katika bifu kubwa baada ya 50 Cent kuahidi kuchangia dola 750,000 kwa hisani ikiwa Mayweather ataweza kusoma ukurasa mmoja wa kitabu cha Harry Potter. 

    Mayweather, ambaye hajapoteza pambano akiwa na umri wa miaka 37, anaendelea na mazoezi mjini Las Vegas, ambako pambano lake litafanyika Mei 2

    Katika kujibu mapigo, mkali huyo a kutupa makode akatweet picha za cheki zake mbili alizolipwa mara ya mwisho, zote zikiwa na jumla ya thamani dola Milioni 70, kumkumbusha 50 Cent alikuwa ana utajiri kiasi gani.
    Uhusiano wa Mayweather na 50 Cent ulikuwa wa kibiashara hadi mwaka 2012 walipozinguana na baadaye akaanzisha kampuni yake mwenyewe.
    Mayweather na Pacquiao wote walianza mazoezi juzi, mjini Las Vegas na Los Angeles kujiandaa kwa pambano hilo na wanatarajiwa kukutana katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Los Angeles Machi 11 kuzungumzia pambano hilo. 
    Pacquiao trained in the Philippines before jetting to Los Angeles to continue his preparations
    Pacquiao akijifua nchini Ufilipino kabla ya kwenda Los Angeles kuendelea maandalizi yake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 50 CENT AWEKA DOLA 'MILIONI NA UPUUZI' MAYWEATHER ATAMDUNDA PAQCUIAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top